Tuesday, July 9, 2013

MASHINDANO YA RAMADHANI SUPER CUP 2013 KATA YA CHAMAZI KUANZA RASMI HAPO KESHO YAKIWA NA BARAKA ZOTE ZA TEFA, TIMU 16 ZATHIBITISHA KUSHIRIKI.

Mashindano ya Ramadhani Super Cup Kata ya Chamazi yanatarajiwa kuanza rasmi hapo kesho tarehe 10 Julai, 2013 yakiwa na lengo la kutoa burudani ya mpira wa miguu kwa wakazi wa Kata ya Chamazi iliyopo wilayani Temeke nje kidogo mwa jiji la Dar es salaam kwa kipindi chote cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mashindano haya yanafanyika kwa mara ya kwanza katika kata ya Chamazi ikishirikisha timu mbalimbali kutoka Kata hiyo, huku timu kumi na sita tayari zimeshajisajili na kukubali kushiriki katika mashindano haya yanayotarajiwa kutoa bingwa siku ya sikuu ya Iddi itakayotegemea muandamo wa mwezi.

“Mashindano haya yanayotarajiwa kuwa na upinzani mkali kutoka kwa timu shiriki, yatazinduliwa na Mgeni Rasmi ambae ni Diwani wa Kata ya Chamazi lakini pia ni mlezi wa Mashindano Mh. John Lawrence Gama. Timu zote kwa sasa zipo katika maandalizi ya mwisho tayari kabisa kuanza kuonyesha ufundi wao katika mashindano haya yanayongojewa kwa hamu na wakazi wa Chamazi na maeneo ya jirani” Alisema Sady Mrope, Muanzilishi na Mratibu wa Ramadhani Super Cup.

Timu zimegawanywa katika makundi manne, yenye timu nne kwa kila kundi, ambapo kila kundi litatoa timu mbili kuelekea hatua ya mtoano. Timu 16 zitakazoshiriki katika Mashindano haya ni Boda Boda FC, Chamazi FC, Chamazi Islamic, Chamazi United, Fahari, FC Zarau, Inkaza, Kazembe, Magole, Mchele Koka, Mzux Family, Roma, St. Emmanuel, Vigoa, Wakali wa Rodi na Yatima. Huku mshindi wa Kwanza anatarajiwa kunyakuwa Jezi Seti Moja na mshindi wa pili atajinyakulia Mpira Mmoja.

Akiyataja malengo ya Mashindano haya, Mratibu wa Mashindano alisema kwamba Ramadhani Super Cup kiujumla ina malengo Mengi kubwa zaidi ni Kutenge
neza jamii yenye umoja kwa wakazi na viongozi wake. “Malengo mengine ni Vijana kuwa karibu na viongozi wetu, Kukuza vipaji vya vijana, Kudumisha umoja na mshikamano, Kuhimiza vijana kutunza Afya zao, pamoja na kutoa burudani” aliongezea Bw. Mrope.  

“Kwa upande wa Maandalizi tuko vizuri sana na tungependa kuchukua nafasi hii mimi na wenzangu kuwashukuru viongozi wote wa wilaya tuliyowafikia kwa ushirikiano wao wa dhati juu ya kutoa vibali kwa mashindano haya kuanzia Serikali ya Mtaa wa Msufini na Kata ya Chamazi, Diwani wa Kata ya Chamazi kwa utayari wake kushirikiana nasi na kusaidia Zawadi ya mshindi wa kwanza, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chamazi kwa Kutukubalia kutumia uwanja huo, lakini pia Halmashauri ya Wilaya ya Temeke Idara ya Michezo na pia Chama Cha Mpira wa Miguu Wilayani Temeke” Bw. Sady Mrope alisema.

Aidha Muasisi na Mratibu wa Mashindano haya Ndugu Sady Mrope ambae ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam akisoma shahada ya Elimu ya Michezo, ameamua kujitolea kuweza kulisaidia soka la Tanzania Kusonga Mbele kwa kuanzia ngazi ya Chini kabisa ya kata na kuwataka wataalamu wengine wa Elimu ya Michezo wasaidie jamii yao katika kutambua umuhimu wa Michezo kwani ni moja katika ya nyenzo nzuri ba Muhimu ya Ajira, kujenga umoja na kuimarisha afya kama ikitumiwa ipasavyo. 

Pia amewaomba wakazi wa Maeneo ya Mbagala na vitongoji vyake, Chamazi na Mbande kuhudhuria kwa wingi katika kila mechi ili kuweza kutoa hamasa kwa timu zao.

No comments:

Post a Comment