Kamishna wa polisi kanda maalum Dar es salaam Suleiman Kova
Jeshi la polisi kanda maalaum Dar es salaam
linamshikilia mfanyabishara mmoja kwa tuhuma za kuwagonga na gari kwa makusudi watu sita na kuwasababishia majereha huku mmoja akiwa mahututi kwa sababu
ya wivu wa mapenzi.
Akielezea tukio hilo la aina yake kamishana
wa polisi kanda maalum suleiman kova amesema tukio hilo lilitokea katika eneo
la bahari beach kwenye baa iitwayotwayo Kilongawima resort wakati alipokuwa na
rafiki wake wa kike.
Kamishna amesema bwana Heven akiwa na
rafiki yake huyo wa kike aliyetambulika kwa jina la Jovita alihama meza na
kuhamia katika meza ya jirani walipokuwa wamekaa wanaume sita na alipojaribu
kumuita wanaume hao walimcheka na kumdhihaki bwana heven.
Bwana Heven kuona anadhaulika alichukua
gari yake yenye namba za usajili T 546 BXX aina toyota hilux na kuwagonga watu
hao sita na kuwasababishia majerha na mmoja kulazwa akiwa mahututi huku
msichana jovita akitokomea pasipo julikana na mtuhumiwa baada ya tukio hilo
alijaribu kujiua lakini alizuiliwa
walipata mkasa huo wa kugongwa na bwana
Heven Mmari ni Solomon kirato,Peter Marwa,Yahaya Albert ,Noah Mmari na wengine
ambao hawajajulina na wamelezwa katika
hosptali ya Moi baada ya kupata majeraha ya kuvinjika vunjika na wengine kuumia
sehemu za kichwana.
wakati huo huo jeshi lapolisi kanda maalum
linawashikilia majambazi watatu baada kukamatwa huko ilala wakiwa wakiwa
na bastola aina ya Bereta ikiwa na
risasi nane kwenye magazine na risasi zingine tano wakiwa wameficha kwenye pakiti ya sigara ,watuhumiwa hao ni Emmanuel Muya
miaka 30 mkazi wa Mbagala ,Ahamed Abdalah miaka 20 mkazi wa karata ,Jasmini
Rajabu au Asha ambaye ni mama Lishe na mkazi wa Mbagala.
Watuhumiwa hawa pia wamekamatwa na pikipiki
aina ya boxer T 836 CLA .
Wakati majambazi hao wakikamatwa jeshi hilo
pia limefanikiwa kukamata malighaf bandia za kutengenezea pombe kali aina ya
konyagi .
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 28/6/2013
huko wilaya yaTemeke Yombo Buza mtaa wa capetown ambapo polisi walikamata
mtuhimiwa January Kimaro mfanyabiashara na mkazi wa Buza capetown akiwa na
pakiti tupu zipatazo 50 za konyagi ,chupa tupu za konyagi 10 na spirit lita 10
ikiwa ni vifaa vya kutengeneza pombe haramu bandia aina ya konyagi ,mtuhumiwa
anaendelea kushikiliwa na kuhojiwa.
Katika tukio lingine kamishana Suleiman
Kova amesema jeshi hilo limewafanikiwa kuwakamata watuhumiwa 28 kwa tuhuma za
kukutwa na pombe haramu ya Gongo lita 100
huko katika maeneo ya Mchambawima,mkwajuni,kigogo mwembe jando na kigogo
mwembe sindano maeneo haya yote yapo katika wilaya ya kinondoni katika jiji la
Dar es slaam na watuhumiwa waliokatwa ni Ally Shomari ,Mohameds Ahamed na
watuhumiwa wengine 26 ambao wote watapelekwa mahakamani upelezi utakapo
kamilika.
Kamishina wa polisi kanda maaluma amemaliza
kwa kuwashukuru wananchi wote,jeshi la ulinzi la wananchi Tanzania ,idara ya
usalama wa Taifa ,wanahabari kwa kufanikisha kuimarisha ulinzi wakati wa
ujio wa marais wa nchi 14 na wake zao pamoja na wakati wa ujio na kuondoka kwa
rais wa marekani Barack obama kwani hawakuona mabango wala vipeperushi au maandamo ya kupinga ujio wa Rais wa Marekani Barack
Obama.
No comments:
Post a Comment