Picha ya mchoro wa jengo jipya la (MUHAS), litakavyokuwa baada ya kujengwa.
Na Belinda Kweka- MAELEZO
CHUO Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), kipo katika mpango wa kujenga Chuo kipya kwa ajili ya ufanyaji mazoezi kwa wanafunzi.
Ujenzi huo, unatarajiwa kuanza Agosti mwaka huu katika eneo la Mloganzila, Kibamba ambapo, ukimalizika utachukua wanafunzi 15,000 watakaosoma taaluma mbalimbali za afya.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kwenye Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J. K Nyerere jijini Dares Salaam (sabasaba) ,Afisa Mipango Mkuu wa chuo hicho Ulimbaga Kijobile alisema uamuzi huo umetokana na ongezeko la wanafunzi ni wengi.
Alisema eneo hilo lita wezesha wanafunzi hao kupata sehemu za kusomea kwa ufanisi kama vile ya maabara za kisasa, madarasa, na sehemu za ufanyaji mazoezi.
“Tumeamua kuanzisha mradi kwa kujenga chuo kipya kwa sababu MUHAS ina sehemu ndogo na hatuwezi kuipanua kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa chuo ili kuweza kutosha kwa wanafunzi” alisema Kajobile.
Aidha alisema wanafunzi hao , walikuwa wakipata tabu katika kufanya mazoezi ,hivyo hulazimika kwenda hospitali za Mwananyamala na Amana.
“Muda mwingine tunatumia hospitali nyingine ili kupata sehemu ya kutosha lakini hospitali hii itakayojengwa itasaidia kuchukua wanafunzi wote ili kuweza kufanya mazoezi yao bila usumbufu” alisisitiza Ulimbaga.
Alisema ujenzi wa chuo hicho, kinakadiriwa kujengwa ndani ya mwaka mmoja,ambapo wanafunzi wa muhula wa kwanza wa mwaka 2015 wanatarajiwa kuanza.
Aliongeza kuwa kitatoa huduma za kiafya kama hospitali nyingine hivyo wananchi wa eneo hilo wanashauriwa kufika mara baada ya ufunguzi wa chuo hicho ili kupata matibabu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment