Wednesday, July 3, 2013

Serikali yakabidhiwa rasmi Uwanja wa Taifa


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kulia), akimshuhudia Balazo wa China hapa nchini, Balozi Lu Youging akiweka saini katika hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Taifa. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija - Maelezo)
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga (kushoto), akitia saini katika hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma HAB Mkwizu.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (katikati), akishuhudia Balazo wa China hapa nchini, Balozi Lu Youging akibadilishana hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Taifa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangaraka (kulia), akipokea ufunguo wa mfano kutoka kwa Balazo wa China hapa nchini, Balozi Lu Youging kuashiria kukabidhiwa rasmi kwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu (kushoto), akifafanua jambo kwa baadhi ya viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya sherehe ya makabidhiano ya Uwanja wa Taifa, kukamalizika, Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Assah Mwambene (kulia), akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, walipokutana katika sherehe za makabidhiano ya Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment