Wednesday, July 31, 2013

Waziri Dk. Fenella awaasa Vijana wajitambue na kuwa na uthubutu

Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara akizungumza na washiriki wa kambi ya vijana leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo ambayo imeanza tarehe 29 na inatarajiwa kumalizika tarehe 2 Agosti.Kambi hiyo ya vijana ya Dunia imeandaliwa na taasisi isiyo ya Kiserikali International Youth Fellowship(IYF) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Baadhi ya washiriki wa kambi ya vijana wakisikiliza hotuba ya Mheshimiwa Waziri Fenella Mukangara hayupo pichani alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa kambi ya vijana wakisikiliza hotuba ya Mheshimiwa Waziri Fenella Mukangara hayupo pichani alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha sanaa kutoka IYF wakicheza muziki wa kitamaduni kutoka Korea mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara wakati wa hafla ya ufunguzi kambi ya vijana leo jijini Dar es Salaam 

Waimbaji wa Kwaya ya kimataifa kutoka Korea Gracias wakiimba wakati wa hafla ya ufunguzi wa kambi ya vijana l;eo jijini Dar es Salaam.
 Kikundi cha sanaa kutoka Tanzania wakionyesha mchezo wa Tai Kondo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara akiteta jambo na Mkurugenzi wa IYF Tanzania Pastor Joen Hee Yong (katika) kushoto ni mwanzilishi wa IYF Duniani Pastor Park Ock Soo.
Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara akifurahia kwaya ya Gracias ilipokuwa inaimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Profesa Elisante Ole Gabriel. (Picha zote na Frank Shija - Maelezo)

Na Frank Shija - Maelezo
VIJANA nchini wameaswa kujitambua na kuthubutu kwa malengo chanya pamoja ikiwa ni pamoja na kujituma kufanya kazi  zikiwemo za kujitolea kwa kuwa kwa kufanya hivyo wataweza kujikwamua na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenella Mukangara alipokuwa akifungua kambi ya dunia ya vijana leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Fenella amesema kuwa vijana wengi wamekuwa wakiishi kwa mazoe na kufuata mikomba ambapo ni hatari sana matokeo yake wamekuwa wakijikuta wakitenda tofauti na malengo yao.
Aliongeza kuwa ni wakati sasa kwa vijana kujitambua na kubadilisha fikra zao hili waweze kujiletea maendeleo wao wenyewe baadala ya kulalamika kama ambavyo wamekuwa wakifanya.
“Ni muhimu vijina mjitambue na mthubutu kwa malengo chanya, na muanze kwa kila mmoja wenu kujituma kufanya kazi na wakati mwingine jitoleeni kwa faida ya jamii zenu”. Alisema Waziri Fenella.
Aliongeza kuwa Mungu amewajali vijana Talanta na vipaji tofauti hivyo ni muhimu vikatumika kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla na kuongeza kuwa kujitambua kwa vijana kuendane na uthubutu ili kujikwamu kimaendeleo.
Kwa upande wake mwanzilishi wa IYF duniani Pastor Park Ock Soo amesema kuwa ni faraja kwake kuona vijana wengi wamejitokeza kushiriki kambi hiyo akiamini malengo ya kuanzishwa kwa taasisi yake yamefikiwa kwa kiasi kikubwa.
Pastor Park ameongeza kuwa vijana wanapaswa kubadili fikra na mitazamo yao ili kuenenda na kasi ya kujiletea maendeleo badala ya kulalamika na kusubiri kufanyiwa kazi.

Kambi hii ya vijana ni inafanyika hapa nchini kwa mara ya tano na imeandaliwa na taasisi ya International Youth Fellowship (IYF) kutoka Korea kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Badilisha Fikra ktuoka mtazomo hasi kuw chanya”.

No comments:

Post a Comment