Monday, August 26, 2013

JK AWEKA MALENGO KWA HALMASHAURI YAKE KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI MBILI KUTOKANA NA TUMBAKU


Bw. John Kadutu (JK) amabaye pia ni diwani wa kata ya Ichemba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na waandishi wa habari juu ya fursa za uwekezaji zilizopo katika Halmashauri ya wilaya mpya ya Kaliua mkoani Tabora.

Jumla ya shilingi bilioni mbili zinatarajiwa kukusanywa na Halmashauri ya wilaya mpya ya Kaliua katika Mkoa wa Tabora kutoka vyanzo vyake vya mapato ya ndani kutokana na zaola tumbaku katika mwaka wa fedha 2013/2014.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kaliua, bw. John kadutu alitoa kauli hiyo wakati akiongea na Wandishi wa Habari katika hoteli ya Lakairo jijini Mwanza wiki iliyopita.
Bw. Kadutu alisema kuwa licha ya mapato hayo yanayotokana  na zao hilo la tumbaku, Wilaya hiyo ya Kaliua ambayo imetokana na Wilaya ya Urambo pia inakabiliwa na changamoto mbalimbali hususani Barabara, Umeme, Maji pamoja na Sekta ya Afya.

"Kwa hiyo natoa wito kwa Waandishi wa Habari kuzitangaza pia fursa zilizopo katika Wilaya ya kaliua ambapo kuna hifadhi ya Misitu, upatikanaji wa Asali  pamoja na Kilimo cha tumbaku" alisema Bw. kadutu amabaye pia ni diwani wa kata ya Ichemba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema kuwa halmashauri hiyo ambayo inaundwa na kata kuni na nane pia inakaribisha wakandarasi pamoja na wazabuni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo wilayani humo.

JK sanjari na hayo alisema kuwa Halmashauri ya Kaliua inakusudia kupata mgawanyo wa mali kutoka Halmashauri ya urambo.

"Kazi kubwa iliyopo kwa sasa ni kujenga majengo ya Halmashauri na nyumba za watumishi hali inayowalazimu kwa sasa watumishi wa halmashauri hii mpya ya Kaliua kusafiri umbali wa kilometa 30 kutokana na ukosefu wa nyumba" alisema JK.

No comments:

Post a Comment