Wednesday, August 21, 2013

Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), yaanza kutoa masomo ya elimu juu ya Sayansi ya hali ya hewa nchini


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu utaratibu mpya wa Serikalibkwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), kuanza kutoa masomo ya elimu ya juu ya sayansi ya hali ya hewa nchini kuanzia muhula wa masomo 2013/2014.

Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi Dk.Ladislaus Changía KUSHOTO akifafanua juu ya maboresho katika mfumo wa utoaji taarifa za hali ya hewa nchini katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka  hiyo Dk.Agnes Kijazi na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi Zamaradi Kawawa. (Picha zote na Frank Mvungi, Maelezo)


CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kimefanikisha uanzishwaji wa masomo ya shahada ya kwanza ya sayansi ya hali ya hewa (Bsc. Meteorology) katika chuo hicho, kuanzia muhula wa masomo 2013/14.

Mchango wa Mamlaka katika kufanikisha uanzishwaji wa masomo hayo pamoja na kushiriki katika kuandaa mitaala ya kufundishia, kuhakikisha Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) linatambua uanzishwaji wa shahada hiyo, kutoa wataalamu wa kufundisha kozi mbalimbali na kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya mafunzo ya vitendo kwa wanachuo.

Kuanzishwa kwa mafunzo hayo hapa nchini, ni moja ya utekelezaji wa agizo la mheshimiwa Rais, pia kutatoa fursa kwa idadi kubwa ya watanzania, wageni kutoka nje ya nchi, na watumishi wa Mamlaka kwa ujumla kujiunga na masomo hayo ya juu katika taaluma ya hali ya hewa kwa gharama nafuu.

Kwa upande wa Mamlaka, mafunzo hayo yatasaidia kuokoa gharama kubwa iliyokuwa ikitumika kusomesha wataalamu wa hali ya hewa nje ya nchi. Aidha itasaidia kuongeza idadi ya wataalum wakutosha ikizingatiwa hivi sasa gharama yake itakuwa ndogo kulinganisha na hapo awali.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA 

No comments:

Post a Comment