Thursday, August 29, 2013

Wakala wa Mbegu za Kilimo wajivunia wajivunia mafanikio katika Sekta ya Kilimo


Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Masoko na Usambazaji kutoka Wakala wa Mbeg u za Kilimo Bw. Philemon Kawamala(hayupo pichani). (Picha zote na Fatuma Salum-Maelezo)

Mkurugenzi wa Masoko na Usambazaji wa Wakala wa Mbegu za Kilimo, Philemon Kawamala akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu mchango wa wakala huyo, katika uzalishaji wa mbegu bora za kilimo kwa kipindi cha misimu sita tangu kuanzishwa, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa.

TAARIFA YA WAKALA WA MBEGU ZA KILIMO (ASA) KWA VYOMBO VYA HABARI
Taarifa ya wakala wa mbegu za kilimo wa Taifa (ASA) itazungumzia mambo makuu matatu
·      Mchango wa ASA katika uzalishaji wa mbegu bora kwa kipindi cha misimu sita tangu ianzishwe
·      Aina tano za mpunga aina ya AMMKA (Aina Mpya ya Mpunga kwa Africa) zinazopandwa kwenye maeneo ya nchi kavu (Upland rice)
·      Mfumo mpya  wa kuhamasisha matumizi ya mbegu bora kwa wakulima kutumia mnyororo wa thamani “ASA-APPROACH”
1.                   Mchango wa ASA katika kuzalisha mbegu bora kitaifa
Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) ulianzishwa tarehe 23 Juni, 2006 chini ya sheria ya wakala namba 30 ya mwaka 1997. Pamoja na majukumu mengine jukukumu kubwa la wakala ni kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora nchini. Msimu wa kwanza  wa 2006/2007 wakala ulizalisha tani za mazao mbali mbali 429  ambapo ilikuwa ni sawa na asilimia 2.6 ya soko la mbegu nchini na hadi kufikia 2011/2012 uzalishaji umeongezeka na kufikia tani 5,542 sawa na asilimia 19.79 ya soko la mbegu nchini (angalia jedwali na.1)
 Jedwali namba 1: Uzalishaji wa mbegu wa ASA kuanzia 2006/07 hadi 2011/12.
Msimu
Kiasi cha uzalishaji kwa kilo
Kiasi kilichozalishwa na sekta binafsi kwa kilo
Jumla ya kilo   zilizozalishwa kitaifa
Asilimia ya mchango wa ASA kitaifa
2006/07
429,000
16,097,000
16,526,000
2.6
2007/08
637,000
16,174,000
16,811,000
3.79
2008/09
918,000
10,511,000
11,429,000
8.03
2009/10
1,882,000
14,633,000
16,515,000
11.4
2010/11
3,092,000
23,462,000
26,554,000
11.64
2011/12
5,542,000
28,000,000
28,000,000
19.79
2.                 Aina Mpya ya Mpunga kwa Afrika (NERICA-series)
Kamati ya mbegu ya taifa imepitisha aina tano za mpunga wa nchi kavu aina ya AMMKA au NERICA. Kirefu cha AMMKA ni Aina mpya ya mpunga kwa Africa au kwa kiingereza NERICA”New Rice for Africa” AMMKA  ni jina linalounganisha aina nyingi za mpunga kwenye kundi moja. Aina hizi ni NERICA -1, NERICA-2, NERICA-4, NERICA-5 na WAB450. Kutokana na hali ya mabadiriko ya tabia nchi na hasa ukame, aina hizi zinavumulia sana ukame na zinapandwa kwenye maeneo yanayotegemea mvua kama mahindi. Aina hii itachangia sana katika kuongeza uzalishaji wa mpunga hapa nchini kwani maeneo kama haya ni mengi ikilinganishwa na mabonde ya umwagiliaji au mabonde yanayotegemea mvua. Natumia fursa hii kuwaambia wakulima wa Tanzania kulima aina hizi mpya za mpunga. Kwa wakulima wanaopata mvua za muda mrefu wana nafasi ya kupanda na kuvuna mara mbili kwa mwaka kwani zinakomaa kwa muda mfupi kwa kutumia siku 90 hadi siku 100 shambani.

3.          Mfumo mpya  wa kuhamasisha matumizi ya mbegu bora kwa wakulima kutumia mnyororo wa thamani “ASA-APPROACH”
Mnyororo wa thamani wa zao husika huanzia upatikanaji wa pembejeo, uzalishaji, kuvuna, kuongeza thamani na kuuza kwenye masoko yaliyokusudiwa. Mfumo wa zamani katika kuandaa teknolojia hadi kuifikisha kwa walengwa haukuwa ukiangalia sana mahitaji ya soko. Katika mfumo huu wa ASA  wakulima na wasindikaji wanapewa aina 13 za mbegu ya mpunga na kuzitathimini kuanzia upandaji, utunzaji wa shamba, uvunaji na usindikaji na mwisho wakulima kwa kushirikiana na wafanya biashara huchagua mbegu ambayo wanajua itatoa ushindani kwenye soko na mbegu hiyo huzalishwa kwa wingi ili kukidhi mahitaji yao. Mfumo huu tulianza kuujaribu kwenye zao la mpunga na kuongeza matumizi ya mbegu kutoka tani 60 mwaka 2007 na kufikia tani 1500 mwaka 2012. Katika msimu wa 2012/13 ASA imefanyakazi na vijiji 120 katika kanda ya kati kwenye zao la alizeti ambapo tayari mwitikio kwenye matumizi ya mbegu ya alizeti unaaza kuwa mzuri ikilinganishwa na hapo awali.

No comments:

Post a Comment