Saturday, September 21, 2013

Simba, Mbeya City nguvu sawa, Uwanja wa Taifa, zafungana mabao 2-2


Mashabiki wa Simba, wakifuatilia mchezo kat i ya timu yao hiyo na Mbeya City, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Issa Rashid wa Simba, akitafuta mbinu ya kumtoka Deogratius Julius wa Mbeya City wakati wa mchezo huo.
Issa Rashid wa Simba, akimtoka Deogratius Julius wa Mbeya City wakati wa mchezo huo.
 Deogratius Julius wa Mbeya City, akijaribu kuutoa mpira miguuni mwa Haruna Chanongo wa Simba, wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Betram Mombeki wa Simba, akiumiliki mpira mbele ya Deogratius Julius na Steven Mazanda wa Mbeya City.
Betram Mombeki wa Simba, akiwatoka Deogratius Julius (11) na Steven Mazanda (8) wa Mbeya City.
 Betram Mombeki wa Simba, akiwakwepa Deogratius Julius (11) na Steven Mazanda (8) wa Mbeya City.
Betram Mombeki wa Simba, akijaribu kuupiga kichwa mpira uliokuwa ukidakwa na golikipa David Baruan wa Mbeya City
 Heka heka ikiwa imetokea karibu na lango la timu ya Mbeya City wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa Mbeya City wakishangilia timu yao wakati wa mchezo kati yao na Simba, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.


Haruni Chanongo wa Simba, akijaribu kumpiga chenga Deogratius Julius wa Mbeya City, wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana mabao 2-2. 
Hadi mwisho wa mchezo, matokeo yalikuwa kama yanavyoonekana kwenye ubao wa matangazo, Simba 2, Mbeya City 2.

No comments:

Post a Comment