Saturday, September 21, 2013

Ufunguzi wa Michezo ya Shimiwi Mjini Dodoma leo


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Lephy Gembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wafanyakazi wa Wizara,Idara na Asasi za Serikali(SHIMIWI) uliofanyika leo  katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma,ambapo Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Amos Makala alifungua rasmi michezo hiyo. (Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo)
Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Amos Makala akiwa katika uwanja wa Jamhuri leo mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wafanyakazi wa Wizara,Idara na Asasi za Serikali(SHIMIWI),kulia kwake ni Mwenyekiti wa Shimiwi Taifa Daniel Mwalusamba.
Wafanyakazi wa  Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wafanyakazi wa Wizara,Idara na Asasi za Serikali(SHIMIWI) leo mjini Dodoma.
Wafanyakazi wa  Wizara,Idara na Asasi za Serikali  wakishiriki maandamano ya   ufunguzi  wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wafanyakazi wa Wizara,Idara na Asasi za Serikali(SHIMIWI) katika uwanja wa Jamhuri leo mjini Dodoma.
 Bendi ya watoto  wa shule ya Msingi Santhome wakiongoza maandamano ya wafanyakazi wa  Wizara,Idara na Asasi za Serikali  wakati wa ufunguzi  wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wafanyakazi wa Wizara,Idara na Asasi za Serikali(SHIMIWI) katika uwanja wa Jamhuri leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Amos Makala akikagua timu kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu ya  ufunguzi kati ya Hazina na Ras Dodoma leo katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma katika uwanja wa Jamhuri leo  mjini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo  Prof. Elisante Ole Gabrieli Laizer(katikati) akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bunge wanawake kabla ya kuanza kwa mechi ya ufunguzi leo, katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment