Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipokea bendera ya Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) kutoka kwa mwenyekiti wa baraza hilo anayemaliza muda wake ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana. Dk Nchimbi sasa ni Mwenyekiti mpya wa RECSA ambaye anaiongoza kwa kipindi cha miaka miwili. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana wakiwa tayari kuipokea bendera ya RECSA kabla ya Dk Nchimbi kukabidhiwa bendera hiyo ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa kuliongoza baraza hilo kwa kipindi cha miaka miwili. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Mwenyekiti mpya wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo pamoja na watendaji wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na wananchi mablimbali baada ya kukabidhiwa uenyekiti huo katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Mwenyekiti mpya wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimkabidhi zawadi mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa kuiongoza RECSA ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana. Hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia viti vya mbele) akiwa na watendaji wengine wakuu wa wizara hiyo pamoja na wageni waalikwa wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti mpya wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana. Hafla hiyo makabidhiano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment