Mwanachama mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuelezea kilichotokea hadi kushutumiwa na Kamati Kuu ya chama hicho na kuitwa muhaini pamoja na mwenzake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye yeye amevuliwa nafasi zake zote za uongozi wa chama. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.BlogSpot.com)
mwanachama mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuelezea kilichotokea hadi kushutumiwa na Kamati Kuu ya chama hicho na kuitwa muhaini pamoja na mwenzake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye yeye amevuliwa nafasi zake zote za uongozi wa chama.
Wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakichukua matukio na maelezo ya wanachama hao walionyang'anywa nafasi zao za uongozi katika chama hicho.
Mwanachama mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Kitila Mkumbo akiuonesha kwa waandishi wa habari, waraka aliokiri kuuandaa pamoja na wenzake lwa ajili ya kutafuta mwanachama mwenye uwezo wa kuongoza chama hicho pia wa kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Alisema kuwa suala la kujing'atua kwenye chama chake hicho alichokipigania tokea akiwa na umri wa miaka 16, halipo moyoni mwake kabisa kwani anatamani hata motto wake atakapokuwa mkubwa aje kujiunga na chama hicho alichokitumikia kwa muda mrefu na kusababisha hata wananchi wa Jimbo lake kulala kwenye mapaa ya nyumba na misituni kukwepa kuadhibiwa na askari.
Zitto Kabwe akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kile kinachoendelea kwenye chama chake hicho hivi sasa.
Zitto Kabwe akiwaeleza waandishi wa habari kile ambacho mara kwa mara hushutumiwa na viongozi wake.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari, wakiwa katika mkutano huo, kusikiliza hatu zitakazochukuliwa na Mbunge Zitto Kabwe na pia Dk. Kitila Mkumbo.
Zitto Kabwe akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wao huo.
Baadhi ya waandishi wakiandika habari zilizokuwa zikitolewa na wanachama hao.
Baadhi ya waandishi wa habari pamoja na wananchi mbalimbali wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mbunge Zitto Kabwe na Dk. Kitila Mkumbo kwenye mkutano huo, jijini Dar es Salaam .
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo .
Mbunge Zitto akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo, jijini Dar es Salaam leo.
Mwanasheria wa Zitto Kabwe na Dk. Kitila Mkumbo, Albert Msando, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kwenye mkutano huo, jijini Dar es Salaam .
No comments:
Post a Comment