Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii,Moshi
KLABU ya Mchezo wa Judo chuo cha taaluma ya polisi Moshi (MPA)
imefanikiwa kuchukua ubingwa wa jumla katika mashindano ya kwanza ya
mchezo huo yaliyofahamika kama First Moshi Polisi Academy Judo
Championship 2013.
Katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Chuo cha Polisi kwa
kushirikana na chama cha mchezo wa Judo nchini ilishuhudiwa wachezaji
chipukizi kutoka vilabu vya Korogwe, Kisutu na Moshi Polisi
wakionesha vipaji vyao huku mchezaji wake chipukizi, Andrew Thomae
akiibuka mchezaji bora wa mashindano.
Klabu ya Moshi Polisi ilifanikiwa kuibuka mshindi wa baada ya
wachezaji wake kutawala mapambano ya uzito wa kilo 60, 66, 73 pamoja
na mapambano ya wazi yaani Open huku klabu ya Korogwe ikifanikiwa
kushika nafasi ya pili.
Mchezaji Thomae wa MPA ambaye ndiye chachu ya ubingwa wa MPA, alianza
kuonesha ubabe wake mbele ya mpinzania wake Dola Abeid ambaye pia
anatoka klabu ya MPA akimwangusha mara kadhaa ndani ya dakika 3:34:05
za mchezo.
Thomae pia alifanikiwa kumbwaga mchezaji Abubakar Magogo katika mchezo
wa fainali ambaye awali alimduwaza bingwa wa Judo Afrika mashariki
Geofrey Mtawa kutoka klabu ya magereza Ukonga katika hatua ya nusu
fainali mchezo ambao hata hivyo uliisha kwa Mtawa kurusha lawama kwa
muamuzi kuwa hakutendewa haki.
Akizungumza na Globu ya jamii baada ya mchezo kumalizika, Mtawa alisema kuwa
kimsingi alichokifanya mwalimu wake ni kinyume na sheria za mchezo
kwani alimnyima pointi za wazi ambazo zingepelekea yeye kutangazwa
mshidni kwa kile alichodai kuwa Mwamuzi huyo kuwabeba “Madogo”.
“Huu ni uonevu, pale kilichotokea ni uonevu, mimi nimetumia tekniki za
mchezo nimemnyanyua dogo ndani ya uwanja nikamwangusha chini tena
ameangukia mgongo lakini cha kushangaza mwamuzi ananinyima pointi eti
nimenyanyua nje ya uwanja, hapana mchezo huu hautakuwa kwa staili hii,
wananishushia hadhi yangu,” alisema Mtawa.
Washindi wengine katika mapambano mengine ni Bakari Magogo kilo 60
(MPA), Mohammed Korogombe kilo 73 (MPA), Gervas Chilipueli, kilo 81
(Korogwe), Amina Mohammed mpambano wa wazi (MPA) na Geofry Mtawa kilo
90.
Zawadi katika mashindano kwa mshindi wa kwanza katika uzito wa 60 hadi
90 ni vyeti, vikombe, medali na fedha taslimu ambapo washindi wote
walizawadiwa zawadi zao na mgeni rasmi Kamanda wa Polisi Mkoani
Kilimanjaro, ACP-Robert Boaz.
Mashindano hayo yalidhaminiwa na Mkuu wa Chuo cha MPA, Matanga Mbushi
kwa kushirikiana na kampuni ya Marenga Investment, Ibra Line,
Tanzanite One, pamoja na Benki ya NMB tawi la Mandela .
Washiriki wa mashindano ya mchezo wa Judo wakiwa katika picha ya pamoja.
Wanawake pia walioneshana kazi katika mashindano hayo .
Mwanamuziki wa zamani wa bendi ya Twanga Pepeta Anko Venna akitoa
burudani katika mashindano hayo ,Venna hivi sasa ni miongoni mwa
waongozaji wa Bendi ya Super Kwata International pinayomilikiwa na
chuo cha Polisi.
Mgeni rasmi katia mashindano hayo kamanda wa polisi mkoa wa
Kilimanjaro Robert Boaz(mwenye kofia nyekundu)akifuatilia moja ya
pambano.
Bingwa wa mchezo wa judo Afrika mashariki Geofrey Mtawa wa magereza
Ukonga akijaribu kutaka kumtupa mchezaji Abubakary Magogo wa MPA
katika pambano la wazi ambalo hata hivyo Mtawa alipoteza kwa pointi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akikabidhi zawadi
kwa mshindi wa kwanza wa mchezo wa Judo Geofrey Mtawa wa magereza
Ukonga kwa wachezaji wa uziti wa kilogramu 90.
Mchezaji bora wa mchezo wa Judo katika mashindano ya First Moshi
Poilisi Academy Judo Championship 2013,Andrew Thamae akiwa ameshikilia
vikombe alivyo fanikiwa kutwaa,kulia kwake ni kamanda wa polisi mkoa
wa Kilimanjaro Robert Boaz aliyekuwa mgeni rasmi.
No comments:
Post a Comment