Sunday, December 8, 2013

Maandalizi ya Gwaride la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika


Kikosi cha Wanawake cha Jeshi la Polisi kikiongozwa na Inspekta Latifa Chicco, kikipita kutoa heshima mbele ya jukwaa kuu lililokuwa na baadhi ya viongozi wa Mkoa, Uwanja wa Uhuru, wakati wa mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya Gwaride la Uhuru, Dar es Salaam leo.
Kikosi cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), kikipita mbele ya jukwaa kuu, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo, kikitoa heshima wakati wa maandalizi ya mwisho ya gwaride la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika, inayoadhimishwa keshokutwa, Desemba 9, 2013.
Kikosi cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), kikitoa heshima wakati wa maandalizi ya mwisho ya gwaride la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika, inayoadhimishwa keshokutwa, Desemba 9, 2013.
Kikosi cha Jeshi la Anga, kikipita mbele ya jukwaa kuu la Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, kutoa heshima wakati wa maandalizi ya mwisho ya gwaride la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika, inayoadhimishwa keshokutwa, Desemba 9, 2013.
Kikosi cha Jeshi la Anga, kikitoa heshima mbele ya jukwaa kuu, wakati wa maandalizi ya mwisho ya gwaride la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika, inayoadhimishwa keshokutwa, Desemba 9, 2013.
Kikosi cha Jeshi la Anga, kikitoa heshima mbele ya jukwaa kuu, katika maandalizi ya mwisho ya gwaride la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika, inayoadhimishwa keshokutwa, Desemba 9, 2013.
Kikosi cha Wanamaji, kikitoa heshima mbele ya jukwaa kuu, katika maandalizi ya mwisho ya gwaride la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika, inayoadhimishwa keshokutwa, Desemba 9, 2013.
Kikosi cha Jeshi la Magereza kikipita mbele ya jukwaa kuu la viongozi katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo, kutoa heshima wakati wa maandalizi ya mwisho ya gwaride la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika, inayoadhimishwa keshokutwa, Desemba 9, 2013.
Vijana wa halaiki wakiwa kazini wakati wa mazoezi hayo, ya mwisho ya maandalizi ya maadhimisho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu ratiba ya maadhimisho hayo, pamoja na kuwaelezea wananchi mbalimbali watakaohudhuria kwenye maadhimisho hayo, sehemu za kukaa kwenye Uwanja wa Uhuru pamoja na wakati wa kufika uwanjani hapo. (Picha zote na KassimMbarouk-www.bayana.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment