Sunday, December 8, 2013

Tatizo la Watoto wenye ugonjwa wa vichwa vikubwa na mgongo wazi laongezeka


Afisa Muuguzi msaidizi wa taasisi ya tiba ya mifupa,mishipa ya fahamu na upasuaji wa Ubongo(MOI)katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,akitoa ushauri kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja kuhusina na kula vyakula vyenye fuliki acid ya kutosha kama vile mboga za majani,Matunda,Maharage na Viazi,wakati wafanyakazi hao walipofika kutoa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Tsh Milioni nane(8,000,000)kwa ajili ya watoto wenye ugonjwa wa kichwa vikubwa na mgongo wazi.
Katibu wa chama cha wazazi wa watoto wenye matatizo ya mgongo wazi na kichwa kikubwa (ASBAHT)Bi.Hidaya Juma (kulia)akielezea jinsi mirija inavyoingizwa kichwani wakati wa matibabu ya watoto wenye matatizo hayo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja wakati wafanyakazi hao walipofika kutoa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Tsh Milioni nane(8,000,000)kwa ajili ya watoto wenye matatizo ya kichwa vikubwa na mgongo wazi.
Mmoja wa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,kitengo cha huduma kwa wateja akifurahia jambo na mtoto mwenye tatizo la kichwa kikubwa Ibrahim Haji(4)anaetibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,wakati wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja walipofika kutoa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Tsh Milioni nane(8,000,000)kwa ajili ya watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja Emmy Njau(kushoto) na kiongozi wa kitengo hicho Geoffrey Wilfred(kulia)wakiwafariji baadhi ya watoto wenye ugonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo wazi wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,walipofika hospitalini hapo kutoa msaada wa vyakula na viti vya kutembelea vyote vyenye thamani ya Tsh Milioni nane(8,000,000).
Muuguzi Mkuu wa watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo wazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,Bi.Haulat Daudi akielezea umuhimu wa vifaa maalumu vinavyotumika wakati wa matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo wazi mara baada ya kukabidhiwa na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Bi. Harriet Lwakatare(kushoto)Jumla ya Tsh Milioni nane(8,000,000)zilitumika katika msaada huo.
Mzazi wa mtoto John Winfred wa kwanza toka kushoto aliekaa chini akiwaangalia wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja Bi.Leah Ntisi na Joseph Msafiri (kulia)wanavyomweka sawa mwanae katika moja ya viti vilivyotolewa msaada vyenye thamani ya Tsh Milioni nane(8,000,000)na wafanyakazi wa kitengo hicho kwa watoto wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wenye ugonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo wazi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,Kitengo cha huduma kwa wateja wakifarijiana na wazazi wa watoto wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wenye kusumbuliwa na ugonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo wazi,wakati wafanyakazi hao walipofika Hospitalini hapo kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Tsh Milioni nane(8,000,000)mahususi kwa ajili ya watoto hao.

Imeelezwa kuwa tatizo la watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi limekuwa kubwa zaidi tofauti na jamii inavyolichukulia tatizo hilo. Huku ikibainika zaidi kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa kwa mwaka na ugonjwa huo ni zaidi ya elfu huku 250 tu ndio wanafika katika taasisi ya tiba ya mifupa, mishipa ya fahamu na upasuaji wa Ubongo (MOI)

Hayo yamebainishwa na Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Patrick Mvungi wakati akipokea misaada mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia kampeni ya pamoja na Vodacom inayoendeshwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

“Tatizo la Ugonjwa wa kichwa kikubwa na uti wa mgongo ni kubwa sana katika nchi yetu na linaongezeka siku hadi siku, na tunapenda kuweka wazi kuwa tatizo hili linasababishwa na wakina mama, kuanzia wanapopata ujauzito hadi kufikia kipindi cha miezi mitatu hapa ndipo tatizo linapotokea, alisema, “Katika kipindi hiki mama asipokuwa anakula chakula chenye lishe (Lishe Bora) na kwenda Kliniki kwa wakati inapelekea kupata upungufu wa madini ya Folic acid.” Alisema Mvungi na kuongeza

“Tunahitaji jamii ituelewe na ndipo tunapo hitaji msaada wa wadau wengine kama Vodacom kutuwezesha kuweza kutoa elimu kwa jamii, kwa mfano hali ilivyo sasa, watoto wanaozaliwa na ugonjwa huu kwa mwaka inafikia zaidi ya elfu nne (4000) kwa mwaka, lakini watoto tunaowapokea hapa kwa mwaka wanafikia 250 tu. Ni jambo la kusikitisha sana. Alisema Mvungi na kuongeza.

“Idadi ya watoto wanaozaliwa ukilinganisha na tunaowapokea hapa kwetu ni tofauti kabisa, wengi wanakuwa wanaamini tatizo hili linatokana na mambo ya kishirikina na inapelekea watoto wa aina hii kuuwawa wengine wanafichwa na wazazi wao, tunapashwa kuondokana na hali hii ili tuweze kukabiliana na tatizo hili.” Alihitimisha Mvungi.

Akizungumzia juu ya misaada hiyo yenye thamani ya shilingi Milioni nane Afisa Mkuu  wa Kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Vodacom Tanzania Harriet Lwakatare amesema kuwa kampuni yake itaendelea kuunga mkono sehemu muhimu zinazogusa maisha ya jamii kwani wao ndio wanaowaunga mkono kila siku.

“Tunatambua mahitaji muhimu waliyonayo jamii ya Watanzania, hasa watoto hawa wenye ugonjwa huu wa Vichwa vikubwa na mgongo wazi, Tumeguswa sana na maisha ya watoto hawa na tumejisikia faraja kuwasaidia na kuwafariji, tumefarijika kuwa sehemu ya maisha yao,” alisema Lwakatare.

Kwa upande wake moja ya Wazazi wa watoto hao amesema kuwa amefarijika kupokea misaada hiyo, na kuomba jamii iweze kumsaidia aweze kupata ada ya kuendelea kumsomesha mtoto wake.

“Pamoja na tatizo hili alilonalo mtoto wangu ameweza kujitahidi kusoma hadi kufikia darasa la tatu lakini nimeshindwa kumuendeleza kwa sababu ya kukosa ada ya kuendelea kumsomesha naomba kwa mtu yoyote atakae kuwa na  uwezo wa kunisaidia anisidie japo kumsomesha tu.” Alisema Mzee Joseph Kaza, baba wa motto Selemsni Joseph (13) mwenye ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment