Saturday, January 25, 2014

Kampuni ya China Word Buz yaelezea njia mbadala zitakazopunguza gharama za wafanyabiashara wadogo kufuata bidhaa nchini China‏

1a 
Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo China Bwana Cheng Wang Wu akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Palace jijini Arusha wakati wa semina na waandishi hao kuhusu mfumo wa kampuni hiyo utakaosaidia wafanyabiashara wadogo wa Tanzania kutafuta soko la bidhaa nchini China na kuwapa taarifa sahihi za masoko kwa msaada wa kampuni hiyo,Mfumo huo hautampa gharama kubwa mfanyabiashara kama vile Usafiri , Chakula, Hoteli.kwani hatalazimika kusafiri kwenda China ili kununua bidhaa badala yake kampuni hiyo itamuagizia na kumfikisha mahali alipo ama kumshauri ni njia gani anaweza kutumia kupata bidhaa kutoka China, kulia ni Shafii Mwaijande Ofisa Mtendaji Mkuu wa China Word Buz kwa upande wa Tanzania.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-ARUSHA) 2 
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda akifafanua jambo wakati wa semina hiyo kwenye hoteli ya Palace jijini Arusha, kulia ni Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo China Bwana Cheng Wang Wu na kushoto ni mmoja wa maofisa wa kampuni hiyo China. 3 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande akionyesha kipeperushi kinachoelezea moja ya makampuni makubwa ya bishara ambayo yamesaini mikataba ya kibiashara na kampuni ya China World Buz, katikati ni Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo China Bwana Cheng Wang Wu na wa pili kutoka kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda 6  
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda akielezea mfumo ambao kampuni hiyo itautumia kuwagizia bidhaa za wafanyabiashara ambao hautampa gharama kubwa mfanyabiashara kama vile Usafiri , Chakula, Hoteli kwani hatalazimika kusafiri kwenda chini ili kununua biashara badala yake kampuni hiyo itamuagizia na kumfikisha mahali alipo, Katikati ni Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo China Bwana Cheng Wang Wu na kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande 7 
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda akielezea mfumo wa soko kwa Watanzania nchini China kwa sasa ambao unawapa gharama kubwa wafanyabiashara. 8 
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika semina hiyo
1 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande akitambulisha kampuni hiyo kwa waandishi wa habari jijini Arusha  wakati wa semina hiyo.

No comments:

Post a Comment