HIVI karibuni, watangazaji nyota waliojizolea umaarufu mkubwa Bongo kupitia Redio Clouds FM, wakitangaza kipindi cha XXL, Hamisi Mandi ‘B12’ na Adam Mchomvu ‘Baba John’ walisimamishwa kazi kituoni hapo kwa muda usiojulikana.
Inaelezwa
kuwa, hata yule mtangazaji mwenye sauti yenye mvuto wa aina yake Fatuma
Hassan ‘Dj Fetty’ naye yupo kifungoni muda mrefu kabla ya akina B12
ingawa taarifa hizo hazijathibitishwa rasmi.
Katika
mkumbo wa akina B12, mtangazaji mwingine wa Kipindi cha Ala za Roho,
Loveness Malinzi 'Diva Loveness Love' naye amesimamishwa.
Uamuzi
wa kuwasimamisha B12 na Mchomvu ulifikiwa na uongozi wa Clouds kupitia
Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti wa Kampuni ya Clouds Media Group, Ruge
Mutahaba kwa maelezo kwamba, wamekwenda kinyume na utaratibu wa kazi
ambao unaonesha vizuri kwenye mikataba yao.
Pigo
hilo limekuwa nafasi ya kutoka jumla kwa kijana Raymond Mshana ambaye
kwa hakika anatumia nafasi hiyo vizuri sana. Raymond hutangaza Kipindi
cha Top 20 kinachoruka hewani kila Jumapili kituoni hapo.
Kama
ni msikilizaji wa Kipindi cha XXL kinachoruka hewani kupitia redio hiyo
kila siku (kuanzia Jumatatu – Ijumaa) tangu mishale ya saa 7 mchana hadi
saa 10 alasiri, utakubaliana nami kuwa jamaa anajua anachokifanya.
Jambo
la msingi kwa Raymond ni kufahamu kuwa uwezo anao, aongeze bidii zaidi
ili aweze kupata nafasi kubwa zaidi ya kuonyesha uwezo wake. Watu
wanaweza kuona shoo zinapwaya kwa namna ama nyingine lakini si kwa ubora
wa kazi – ni mazoea ya sauti za kila siku.
Sishabikii
akina B12, Dj Fetty na Mchomvu kuwa nje ya vipindi hivyo na ni
matarajio yangu kuwa watarejea hivi karibuni lakini iwe changamoto kwa
Mshana mwenyewe, kuendelea kukaza ili azidi kuwa matawi ya juu.
Wengi hawamfahamu japo kwa ufupi. Hapa nitakueleza japo kidogo sana ili upate kumfahamu Raymond.
NI NANI HASA?
Anaitwa Raymond Mshana (25), mzaliwa wa Same, Kilimanjaro. Raymond ni
Mpare, moja ya makabila maarufu sana nchini. Wapare hutaniana na Wachaga
ambao wote ni kutoka mkoani humo. Katika utani wao, Wachaga wamekuwa
wakiwatania Wapare kuwa ni wabahili sana! Tehe...
(HABARI NA JOSEPH SHALUWA/GPL)
No comments:
Post a Comment