Friday, February 14, 2014

KONGAMANO LA UWEKEZAJI KANDA YA ZIWA LAENDELEA LEO KWA SIKU YA PILI JIJINI MWANZA


 Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama (liesimama) akitoa muongozo wa namna vikao vitakavyokuwa vinaendelea kufanyika katika kumbi mbali mbali ndani ya Hoteli ya Malaika,iliwa ni muendelezo wa Kongamano Uwekezaji Kanda ya Ziwa,unaoendelea kufanyika leo kwenye Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.Wengine pichani toka kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye ndie Mwenyeji wa Kongamano hilo,Mh. Everist Ndikilo,Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh. Charles Kitwanga pamoja na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopha Chiza.
Mwenyekiti wa Kikao kinachojadili maswala ya Ufugaji katika Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kikao hicho (hawapo pichani) wakati akitoa muongozo wa kikao hicho kinachoendelea kufanyika hivi sasa katika Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mh. Said Magalula na Kulia ni Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Bw. Fanuel Lukwaro
Mtoa Mada iliyohusu Fursa za Uwekezaji katika Ufugaji na Michakato ya kuwa na Machinjio bora,Prof. Lazaro Kurwijila kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (Idara ya Sayansi ya Wanyama) akisisitija jambo wakati akiwasilisha mada yake hiyo,kwenye Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa EPZA,Dkt. Adelhelm Meru akifafanua jambo wakati akielezea namna EPZA inavyofanya kazi kwa wawekezaji mbali mbali.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye ndie Mwenyeji wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. Everist Ndikilo akifatilia kwa makini kikao hicho kinachoendelea kufanyika hivi sasa katika Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.
Wajumbe wakifatilia kikao hicho.
Mwenyekiti wa Kikao kinachojadili maswala ya Kilimo katika Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopha Chiza (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Kikao hicho (hawapo pichani) wakati akitoa muongozo wa kikao hicho kinachoendelea kufanyika hivi sasa katika Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinganga,Mh. Yohana Balele.
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),Mh. Aggrey Mwanri (wa pili kulia) akiwa pamoja na Wajumbe wengine kufatilia moja ya vikao vinavyoendelea kwenye Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.
Wajumbe wakipitia makabrasha mbali mbali ya Kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akizungumza wakati akiwasilisha mada yake iliyohusu uwepo wa Fursa za Uwekezaji katika Uwindaji na Hoteli wakati wa Kikao kilichokuwa kikijadili maswala ya Miundombinu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Elimu na Afya katika Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Dkt. Aloyce Nzuki akiendelea kutoa mada yake.
Sehemu ya Wajumbe kutoka sekta mbali mbali wakifatilia kwa umakini vikao hivyo.Picha zote na Othman Michuzi,Mwanza.

No comments:

Post a Comment