Wednesday, February 19, 2014

Watangazaji,Wanamichezo na Wasanii wa Filamu nao wameletewa Tuzo zao.


Print
Kwa sasa Tanzania itapata nafasi nyingine ya kushuhudia tuzo zitakazotolewa kwa ajili ya watu ambazo hizi zinaitwa Tanzania People’s Choice Awards,hii inahusisha wale wote unaowapenda kwenye tasnia ya Utangazaji wa Tv na Redio,Wasanii wa Filamu,Wanamichezo na Muziki.
Tuzo hizi zitakuwa zikisimamiwa na Bongo5.com ambap0o wanasema mwaka 2009 liliwajia wazo jipya,wazo la kuwa na tuzo zitakazopatikana kwa mchakato wa wazi utakaotokana na mapendekezo ya watu wenyewe ya kuchagua mastaa wa michezo, muziki, filamu au vipindi na watangazaji wanaopendwa zaidi.
Wazo hilo liliendelea kuboreshwa na mwaka huu (2014) limeiva na liko tayari kutoka kwenye hatua ya wazo la kichwani na kuwa tukio lenyewe’.
Mwenyekiti wa Bongo5 Media Group Luca Neghesti amesema>>”Nilizisajili na kuanzisha mwaka 2009 ila kutokana na mipango na malengo ya kampuni niliamua kuziweka kwanza hadi sasa,Sasa hivi tumeshuhudia ukuaji katika
tasnia mbalimbali na tumeona ni wakati muafaka wa kuwatunuku wale wanaopendwa na wananchi, kuwapatia tuzo pamoja na zawadi ya fedha taslimu’
‘Tofauti na tuzo zingine tuzo za watu hazitafuti ubora bali zinalenga wanaopendwa zaidi na tuzo hizi hazitajikita katika tasnia moja peke yake,Kwa kuanzia tuzo hizi zitatolewa katika tasnia ya burudani inayojumuisha
filamu na muziki’.
Tuzo hizi Pia zitaiangazia sekta ya utangazaji kwa kuwatunuku watangazaji na vipindi vinavyopendwa zaidi na watu nchini huku pia mwanamichezo bora (soka, basketball, ndondi na michezo mingine) naye akipewa nafasi,na kingine ni kwamba tuzo za watu si tuzo za vijana peke yake, zipo kuwakilisha watu wa rika zote.
Nimeambiwa utofauti mwingine mkubwa ni kuwa tuzo za watu zinalenga kuwatunuku watu kutokana na umaarufu ama kupendwa kwao na si ubora na hazitakuwa na ushindani na tuzo0 zingine kwa sababu hazilengi tasnia moja tu.
Upigaji kura unaanza wiki hii katika vipengele 11 ambapo wananchi wenyewe watachagua majina ya washiriki watakaoshinda,awamu ya kwanza ya upigaji kura itafungwa baada ya wiki mbili kutoka siku ya kwanza ya upigaji kura na majina ya watu watano waliotajwa zaidi kutoka kwenye kila kipengele watachaguliwa kama watajwa wa mwisho.
Kuanzia hapo upigaji kura wa wananchi utajikita tu katika orodha ya majina hayo matano kwenye kila kipengele kinachoshindaniwa,Wiki moja baada ya majina ya washiriki kutangazwa, mchujo wa kwanza utafanyika katika kila kipengele na mtu mmoja ataondolewa.
Wiki moja baadaye mchujo wa pili utafanyika na kuwabakiza washiriki watatu kwenye kila kipengele ambao jumla watakua  33 wao watakuwa wageni wa heshima kwenye utoaji wa tuzo hizo.
Na tunzo hizi zitafanyika wiki moja baada ya mchujo huo wa mwisho katika hafla hiyo washindi watatangazwa na kila mshindi atapokea zawadi ya fedha taslimu ambazo ni T.shilingi 1,000,000 za Kitanzania pamoja na tuzo ya thamani
iliyotengenezwa kwa mkono kutoka kwenye mali ghafi asili za Kitanzania.
Tuzo za watu mwaka 2014 zitajumuisha vipengele 11 ambavyo ni pamoja na:
  1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW1 na jina’ kwenda
    15678)
  2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW2 na jina’ kwenda
    15678)
  3. MTANGAZAJI WA TV ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW3 na jina’ kwenda 15678)
  4. KIPINDI CHA TV KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW4 na jina’ kwenda 15678)
  5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW5 na jina’ kwenda 15678)
  6. MWANAMUZIKI WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW6 na jina’ kwenda
    15678)
  7. MWANAMUZIKI WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW7 na jina’ kwenda
    15678)
  8. WIMBO UNAOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye ‘TZW8 na jina’ kwenda 15678)
  9. MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW9 na jina’
    kwenda 15678)
  10. MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW10 na
    jina’ kwenda 15678)
  11. FILAMU INAYOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye ‘TZW11 na jina’ kwenda 15678)
JINSI YA YA KUPIGA KURA
Mchakato wa kupendekeza majina ya washiriki katika tuzo hizi utafanyika kwa njia kuu mbili,ya kwanza ni kwa kutumia tovuti ya  tuzo hizi ambayo ni www.tuzozetu.com ambapo utakutana na hatua rahisi ya kupendekeza na
kutaja majina katika vipengele vyote 11.
Jinsi ya kupiga kura, bofya palipoandikwa  Piga Kura na ufuate hatua rahisi kabisa ambayo haikuhitaji
kujiandikisha jina wala email yako,njia ya pili ni kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi[sms]ambapo utaandika neno ‘Tuzo’ kwenda namba 15678.
Baada ya kuandika hivyo utaletewa menu yenye vipengele vyote 11 vikiwa na code number zake kutaja ama kupendekeza jina,utatuma code husika na jina kwenye namba hiyo hiyo kwa mfano  Justin
Bieber.

No comments:

Post a Comment