Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kijiji cha Wangama,
Fred Mgata (kulia) akikabidhi kadi za chyama hicho kwa Katibu wa CCM
Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga baada ya yeye na wanachama wengine 50 wa
Chadema kuamua kukihama na kujiunga CCM katika mkutano wa kampeni za CCM
uliofanyika katika Kijiji hicho kilichopo Kata ya Luhota, Iringa
Vijijini leo. Mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chadema ambaye
ni mzaliwa wa kijiji hicho, Grace Tendega alikuwa chini ya uongozi wa
Mgata.
Mgata akisalimiana na mgombea wa CCM Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa
Mgata akipongezwa na wafuasi wa CCM kwa kitendo chake cha kuamua kuihama Chadema na kujiunga na CCM
Ofisa wa Umoja wa Vijana wa CCM Makao Makuu, Mariana Shonzaakimuombea kura mgombea ubunge wa CCM, Mgimwa.
Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akihutubia katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Wangama.
Mgombea
ubunge Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey
Mgimwa 9kulia) akilakiwa kwa shangwe na vigeregere na wananchi wa Kijiji
cha Ikuvilo, Kata ya Luhota alipowasili kwa ajili ya mkutano wa kampeni
za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo leo Iringa Vijijini.
Mgombea
ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (wa pili kushoto) na
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu wakiungana na
wananchi wa Kijiji cha Wangama alichozaliwa mgombea ubunge wa Chadema,
Grace Tendega, wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata ya Luhota,
Iringa Vijijini leo.
Baadhi
ya mabalozi wa CCM wa Kijiji cha Wangama wakinyoosha juu mikono ikiwa ni
ishara ya kukubali kumpigia kura mgombea ubunge Jimbo la Kalenga
kupitia chama hicho, Godfrey Mgimwa, wakati wa mkutano wa kampeni za
uchaguzi mdogo wa jimbo hilo utakaofanyika Machi 16, mwaka huu.
Mkazi wa Kijiji cha Wangama akifurahia sera za CCM zilizokuwa zinatolewa kwenye mkutano huo.
Katibu
wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Arusha Mjini, Rehema Mohamed
akionesha moja ya majeraha yaliyvyomuathiri mguuni wakati wa vurugu
zilizofanywa katika maandamano ya Chadema mkoani Arusha. Rehema ambaye
kabla ya kuhamia CCM alikuwa Diwani wa Chadema, alikuwa akihutubia
katika mkutano wa kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM,
Godfrey Mgimwa leo katika Kijiji cha Ikuvilo, katika Kata ya Luhota,
Iringa Vijijini leo.
Mfuasi
wa CCM, Sabinus Segerela akishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya
mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa katika mkutano wa
kampeni katika Kijiji cha Ikuvilo, Kata ya Luhota, Iringa Vijijini leo.
Katibu wa
Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, Seif Shaaban Mohamed, akihutubia katika
mkutano wa kampeni za CCM za kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga,
Godfrey Mgimwa katika katika Kijiji cha Ikuvilo, Kata ya Luhota, Iringa
Vijijini leo. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
No comments:
Post a Comment