Zaidi
ya shilingi milioni 65 zimekusanywa katika harambee iliyoongozwa na
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwa ajili ya kuchangia ujenzi
wa ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililoko jijini Dar
es salaam.
Kati
ya fedha hizo zilizokusanywa katika ibada maalum ya kuchangia ujenzi wa
jengo la ukumbi huo ilyoongozwa na Mhadhama Kadinali Polycap Pengo kiasi
cha shilingi milioni 60.5 zilikuwa ni ahadi na shilingi milioni 5
zikiwa ni fedha taslimu.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Makamu wa Rais aliwahakikishia Watanzania kuwa
serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za taasisi za kidini katika
kudumisha amani na upendo ndani ya jamii bila ya kujali tofauti za aina
yo yote ile.
Alisema
kuwepo kwake katika hafla hiyo ni ishara ya uhusiano mkubwa uliokuwepo
kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi mbali
mbali za dini nchini.
“Sisi
Watanzania tumefika hapa kutokana na uongozi thabiti wa waasisi wa Taifa
letu. Hivyo, tunataka nchi ya watu wanaomwogopa Mungu, watu
wanaopendana, watu wanaovumiliana na watu wanaotakiana mema katika
shughuli zao.”
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Mama Rose Rupia kamati yake
inahitaji shilingi milioni 600 zaidi kukamilisha hatua za mwisho za
ujenzi wa jengo la ukumbi huo na kwamba tayari wameshatumia kiasi cha
shilingi bilioni moja katika ujenzi huo.
Ibada hiyo maalum ilihudhuriwa pia na viongozi mbali mbali akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
26/1/2014
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe Benjamin Mkapa,
wakati alipowasili kwenye Kanisa la Mtakatifu Peter Oysterbay, leo
asubuhi kwa ajili ya kushiriki katika Harambee ya kuchangia Ujenzi wa
Ukumbi wa mikutano wa Kanisa hilo. ambapo zaidi ya Sh. milioni 65
zilipatikana kati ya Sh. milioni 600, zinazohitajika hadi ifikapo mwezi
Julai. Kati ya hizo Cash ni Sh. milioni 5 na zilizobakia zikiwa ni
ahadi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na Rais Mtaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, wakishiriki katika Misa
maalum ya Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa
la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi
Jan 26, 2014
Mwadhama
Cardinali Polycap Pengo akiongoza ibada maalum ya Harambee ya kuchangia
ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo
Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuh
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na waumini wakati wa Ibada maalum ya Harambee ya kuchangia
ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo
Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Mwadhama Cardinali Polycap Pengo, wakati wa ibada
maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa
la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuh
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akisalimiana na Mwadhama
Cardinari Polycap Pengo, wakati wa ibada maalum ya Harambee ya kuchangia
ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo
Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuh
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na Rais Mtaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, wakishiriki katika Misa
maalum ya Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa
la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio
Baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu waliohudhuria Ibada hiyo kwenye ibada hiyo.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu waliohudhuria Ibada hiyo kwenye ibada hiyo.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu waliohudhuria Ibada hiyo kwenye ibada hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter,
Stephano Kaombe, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa
Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam,
wakati wa harambee ya kuchangia ujnenzi wa Ukumbi huo iliyofanyika leo
asubuhi
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa wakati
alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa
Kanisa la Mtakatifu Peter, baada ya ibada maalum ya harambee ya
kuchangia ujenzi huo, iliyofanyika leo asubuhi, Jan 26, 2014. Kushoto ni
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter, Stephano Kaombe
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal, akiongoza na na
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, kutoka kanisani baada ya ibada hiyo.
Picha ya pamoja ya kumbukumbu ya siku hii adhimu
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na Rais Mtaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, wakisindikizwa baada ya
kushiriki katika Misa maalum ya Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Ukumbi
wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar
es Salaam. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment