Monday, April 28, 2014

BREAK NEWS : WATU 31 WAFARIKI DUNIA WAKIWEMO ASKARI POLISI WATATU HUKO MKOANI SINGIDA

Watu 31 wamefariki dunia hivi punde nje kidogo ya mji wa Singida baada ya kugongwa na basi ,kati yao wapo askari polisi 3  na raia wapatao 28.

watu hao wamegongwa na basi la SIMUN lilokuwa linatoka  Kahama kwenda jijini Dar es salaam,ajali hiyo imetokea wakati  baadhi yao walipokuwa wakinusuru mwili wa mtu aliyegongwa na gari aina ya Roli.

shuhuda wa ajali hiyo Ally Shemdoe ameimbia blog hii kuwa mtendaji  wa kijiji na mwenyekiti wake ni miongoni mwa marehemu hao 31.

taarifa hii imeletwa kwenu  na mwandishi mkongwe ALLY SHEMDOE kwa taaifa zaidi endelea kutembelea blog hii au wasilian moja kwa moja na mwandishi ALLY SHEMDOE kwa simu namba hii 0755 418 151

blog hii inaungana na watanzania ndugu jamaa na marafiki katika msiba huu mzito Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi na awajalie afya njema majeruhi wapone kwa haraka.

No comments:

Post a Comment