Monday, April 28, 2014

Waziri Nagu azindua Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt. Mary Nagu akizindua Mkataba wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kuzindua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, (kulia) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Regina Kikuli  akimfafanulia jambo Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Packshard Mkongwa wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt. Mary Nagu (mbele mwenye mkoba) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi mara baada ya kuzindua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, (kushoto kwake tai nyekundu) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florence Turuka.

No comments:

Post a Comment