Waziri mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi amewasili katika makao ya wazee ya kanisa katoliki karibu na mji wa Mila kuanza kutekeleza adhabu yake ya huduma kwa jamii.
Alipata adhabu ya kifungo cha miaka minne gerezani mwaka jana ingawa mahakama ikasema kuwa hataenda gerezani bali atahudumia jamii kwa kuwatunza wazee wenye ugonjwa wa 'Denemtia' au ugonjwa wa kusahahu kwa saa nne kila siku.
Alipowasili, alizomewa na mwanaharakati mmoja akiwamwabia kuwa alipaswa kuwa gerezani.Wakuu wa makao hayo wanasema kuwa Berlusconi atakuwa tu kama mfanyakazi mwingine yoyote anayefanya kazi katika makao hayo.
Bilionea huyo amekuwa akikumbwa na kashfa pamoja na kesi nyingi mahakamani.
Hukumu yake mwaka jana ilitokana na kesi ambapo kampuni yake ilinunua haki miliki katika miaka ya tisini.
Lakini aliponea kifungo cha jela kwa sababu mfumo wa sheria nchini Italia unawahurumia sana wazee walio na miaka sabini na zaidi.
Berlusconi aliamua kuhudumia jamii kuliko kuhudumia kifungo cha nyumbani.
Mwandishi wa BBC David Willey anasema kuwa adhabu hiyo itamuwezesha kuendelea kuongoza chama chake Forza Italia, katika uchaguzi wa Ulaya ingawa alilazimika kujiuzulu kutoka katika baraza la Senate.
Berlusconi pia atazuiwa kusafiri katika sehemu nyingi za nchi hiyo baada ya Pasi yake ya usafiri kubanwa.
No comments:
Post a Comment