
Wanawake wa mtaa wa Mlimwa wakimsaidia Mwenzao aiyezilai baada ya Tingatinga la CDA kufika kwa ajili ya kubomoa nyumba yake kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Barabara, zoezi hilo lilifanyika Jana ambapo nyumba zaidi ya 65 zilibomolewa na kuacha familia zaidi ya 150 zikikosa makazi. (Picha zote na Jahn Banda)
Bibi huyu mkazi wa Mlimwa Kusini ambaye hakufahamika jina lake akiwa hajui la kufanya baada ya nyumba yake aliyokuwa akiishi iliyojengwa kwa mtindo wa Tembe huku akiachwa na vyombo vyake alivyoweka kwenye shamba la mahindi baada ya CDA kufanya uvunjaji huo kwa nyumba zote zilizopo katika hifadhi ya Barabara.



Tingatinga la Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) likibomoa moja ya nyumba zilizopo katika hifadhi ya Barabara inayotarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni, ambapo zaidi ya nyumba 65 zilibomolewa katika eneo hilo la Mlamwa Kusini.
Wananchi wa Mlimwa waking'oa mabati muda mfupi kabla ya Tinga tinga la CDA kufika na kuibomoa nyumba hiyo, ili kupisha hifadhi ya Barabara.
Wananchi wa Mlimwa wakihamisha mabati waliyoyang'oa muda mfupi kabla ya Tinga tinga la CDA kufika na kubomoa nyumba yao ili kupisha hifadhi ya Barabara.
No comments:
Post a Comment