Friday, May 9, 2014

Marekani 'inaifungia mlango' Syria

Viongozi wa upinzani wa serikali ya Syria wapo Washington Marekani kwa mashauriano
Marekani imeiwekea vikwazo benki moja ya Urusi inayofanya biashara na Syria kama sehemu ya jitihada za kuzidisha shinikizo za kiuchumi dhidi ya serikali ya Syria.

Hii ni mara ya kwanza Marekani imeiwekea vikwazo benki ya Urussi inayofanya biashara na Syria.Hatua hiyo ilitangazwa wakati viongozi wa upinzani walioitembelea Washington wameanza kukutana na maafisa wakuu wa utawala.
Maafisa wa hazina ya Marekani wanasema hatua hii inanuiwa kuifungia milango Syria isiweze kuendelea kupenya mfumo wa kifedha wa dunia.
Vikwazo zaidi pia vimewekewa viwanda kadhaa vya kusafisha mafuta pamoja na maafisa sita wa ngazi ya juu katia serikali ya Syria.
Hayo yalitangazwa mda mfupi tu kabla ya kiongozi wa upinzani wa serikali ya Syria Ahmad Jarba alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa wa Marekani John Kerry.
Ahmad Jarba yuko katika ziara ya kwanza rasmi huko Marekani ambako anatarajiwa pia kukutana na rais wa Marekani Barack Obama.

No comments:

Post a Comment