Na Francis Dande
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limewataka wafanyakazi wasio katika sekta isiyo rasmi kujiunga na NSSF ili kuboresha maisha yao ya sasa na baadae.
Akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo kwa Makampuni, ambapo NSSF ilikuwa ni miongoni mwa wadhamini Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Said Malawi alisema kuwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), imekuwa ikitoa elimu kwa wanachama wa kupitia huduma ya NSSF Mobile kwenye M-PESA.
Kwa kuwajali wanachama wake NSSF imekuwa ikiwafuata wanachama walio katika sekta isiyo rasmi, mwanachama anaweza kuangalia salio kupitia simu ya mkononi kwa kuandika neno Sajili ikifuatiwa na namba za NSSF zenye tarakimu nane kwenda namba 15747 kisha kuandika neno Salio kwenda namba 15747 na anaweza kupata taarifa za michango aliyotoa. ambapo mwanachama anaweza kuanza kuchangia kuanzia shilingi 20,000 na kuendelea.
NSSF ndio Shirika pekee la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii linalokopesha wanachama wake kupitia Saccos zilizosajiliwa kisheria. Aidha mwanachama anaweza kunafaika na huduma za matibabu ya bure yanatolewa kwa mwanachama pamoja na familia yake wakiwemo watoto wane.
“NSSF inatoa mikopo kupitia Saccos iliyosajiriwa kisheria, iwe inakaguliwa mahesabu yake kupitia Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu aliyehidhinishwa na Serikali”
NSSF pia inauza viwanja vilivyopo katika eneo la Kilunvya vyenye hati miliki ya kudumu, umeme, maji na barabara za kudumu , pia NSSF inauza nyumba zake zilizopo Mtoni Kijichi kuanzia shilingi milioni 64 bila ya VAT.
kulimelililodhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), na kufanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi).
Katika mchezo uliozikutanisha timu za NSSF na Fastjet timu ya timu ya Fastjet iliichapa bila huruma timu ya NSSF kwa idadi ya magori 5-1.
Mshambuliaji wa timu ya NSSF, Mahadhi Mahmoud (katikati) akiwatoka wachezaji wa timu ya Fastjet, Boniface Mwaikelela (kushoto) na Charles Fidelix wakati wa Bonanza la Makampuni la Sports Extra Day ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam jana. Fastjet ilishinda 5-1. NSSF ilikuwa ni miongoni mwa wadhamini wa Bonanza hilo. (Picha na Francis Dande)
Mwanachama mpya wa NSSF akipigwa picha wakati wa zoezi la kuandikisha wanachama wapya lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Huduma za kuandikisha wanachama zikiendelea.
Mwanachama mpya wa NSSF akipigwa picha wakati wa zoezi la kuandikisha wanachama wapya lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Huduma za kuandikisha wanachama zikiendelea.
Ofisa wa NSSF akijiandaa kutoa elimu kwa wanachama wapya.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya NSSF
Wachezaji wa NSSF wakijadiliana wakati wa mapumziko.
No comments:
Post a Comment