Thursday, May 15, 2014

TAARIFA ZA UKAMATAJI WA MAKOSA KITENGO CHA USALAMA BARABARANI KANDA MAALUM KUANZIA 01/05/2014 HADI SASA.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani liliendesha oparesheni kamambe kukamata makosa yanayohusisha uvunjaji wa sheria mbalimbali za usalama barabarani ili kuhakikisha watumiaji wote wa barabara wanazingatia sheria hizo. Makosa hayo ni pamoja na haya yafuatayo:
·         Ubovu wa Magari,
·         Obstraction,
·         Kuzidisha Abiria,
·         T.L.A,
·         Kukatisha Route,
·         Uendeshaji wa hatari,
·         Kutotii Amri,
·         Matumizi mabaya ya barabara,
·         Kutokuwa na Leseni, nk.
Aidha katika oparesheni hiyo vyombo mbalimbali vya usafiri yakiwemo Magari, Pikipiki, Bajaji na vingine vilikamatwa na kutozwa tozo kulingana na makosa kwa kila chombo kama ifuatavyo:
MGAWANYO WA MAKOSA NGAZI YA KI-MIKOA
JUMLA YA MAKOSA - ILALA
JUMLA YA MAKOSA  TEMEKE
JUMLA YA MAKOSA  KINONDONI
JUMLA KUU
3066
2399
4630
10095

MGAWANYO WA TOZO NGAZI YA KI-MIKOA
JUMLA YA TOZO
ILALA
JUMLA YA TOZO  TEMEKE
JUMLA YA TOZO KINONDONI
JUMLA KUU
Tshs 82,200,000/=
65,850,000/=
125,580,000/=
273,630,000/=

Aidha, taarifa ya Kikosi cha Usalama barabarani Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam ya ukamataji wa makosa ya Usalama Barabarani kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Januari 2014 ni kama ifuatavyo:
1.    Idadi ya magari yaliyokamatwa -          64,785
2.    Idadi ya pikipiki zilizokamatwa   -          17,082
3.    Jumla ya Makosa yaliyokamatwa  -      84,474
4.    Fedha za TOZO zilizopatikana     Tsh: 2,534,220,000/=

S.H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment