Na Nathan Mtega wa demashonews,Songea
SERIKALI ya mkoa wa Ruvuma imeendelea kuwasihi wafanyakazi
wa sekta zote nchini wasijenge zaidi utamaduni wa kudai haki bila kutimiza
wajibuwao kwanza kwa sababu kauli mbiu za vyama vingi vya wqafanyakazi kikiwemo
chama cha walimu nchini ambacho kauli mbiu yake
ni wajibu na haki.
Kauili hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Namtumbo Abdula
Lutavi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma kwenye maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Maji maji mjini Songea ambapo
amesema baadhi ya wafanyakazi wakiwemo walimu wamekuwa hawatimizi wajibu wao
ipasavyo lakini ndiyo wanakuwa msitari wa mbele kulaumu na kudai haki pasipo
kutimiza wajibu wao kwanza kwa mwajiri.
Wanafunzi
wa Chuo cha VETA Songea wakipita mbele ya jukwaa kuu huku wakionyesha
mavazi wanayoshona chuoni hapo ikiwemo mavazi la maharusi na ya
ulimbwende.
-----------------------------------
Amesema sekta ya elimu ndiyo yenye watumishi wengi ambao wapo
katika kila kijiji nchini na ndiyo wataalamu wanaotumiwa na wananchi wa maeneo
hayo lakini baadhi yao wamekuwa ni watoro na wazembe katika maeneo yao ya kazi
na kutotimiza wajibu wao kwa makusudi na kwa visingizio mbali mbali na
wakiendelea kulindwa na walimu wakuu pamoja na wakuu wa idara za kielimu hali
ambayo inazidi kudumaza kiwango cha elimu mkoani Ruvuma na kuufanya mkoa
kuendelea kutofanya vizuri katika sekta hiyo muhimu.
Mtangazaji wa TBC mkoani Ruvuma Noela Njawa akipokea zawadi ya mfanyakazi bora
---------------------
Aidha amesema walimu watoro na wazembe ndiyo wanakuwa wa
kwanza kulaumu na kulalamikia masilahi duni na kuhamasisha migomo ambayo
imekuwa ikiwaathiri wanafunzi pasipo sababu huku serikali ikionenesha nia
kuongeza na kuboresha maslahi yao ikiwa ni pqamoja na kulipa malimbikizo mbali
mbali wanayoidai serikali ambayo taratibu za malipo zinaendelea kufanyiwa kazi
na mamlaka husika.
Nao wafanyakazi wa sekta mbali mbali mkoani Ruvuma katika
risala yao kwa mgeni rasmi wameelezea kusikitishwa kwao na kitendo cha taifa
kuadhimidsha miaka hamsini ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar huku taifa
likiwa salama kutokana na dhana iliyojengeka ya kuzingatia utawala bora katika kila Nyanja lakini bado
kumeendelea kuwepo kwa matatizo ya madeni ya watumishi,mishahara duni na
waajiri kutokujali sheria za kazi vitu ambavyo vimekuwa vikiendelea kugonga
vichwa vya wafanyakazi walio wengi na kupunguza morali ya kazi.
Mfanyakazi wa Idara ya wakala wa majengo Mkoa wa Ruvuma Wizara ya Ujenzi Bw. Charles Buhili akipokea zawadi ya mfanyakazi bora.
----------------------
Wamesema imekuwa ni kawaida kwa watumishi wa umma kupewa
ahadi kila mara za kupunguziwa matatizoi yao katika maeneo yao ya kazi
yakiwemon madeni ya muda mrefu ya watumishi hao lakini utekelezaji wa ahadi
hizo umekuwa ni wa kusuasua pamoja hali ya haslisi ya kiuchumi wa taifa
ikijulikana hali imekuwa ikiwavunja moyo watumishi walio wengi wa umma kutimiza
wajibu wao.
Mlinzi wa CCM mkoa wa Ruvuma Bw. Mika Nchimbi akipokea zawadi ya mfanyakazi bora
------------------------
Aidha wafanyakazi katika risala hiyo wametoa maoni kuwa utekelezaji
wa ahadi hizo ungekuwa unapewa uzito kama vile zinavyotolewa kwa msisitizo na
viongozi mbali mbali wa serikali na waajiri kikiwmo kilio cha muda mrefu cha
kodi kubwa kwa wafanyakazi walioko kwenye mfumo rasimi ambao wamekuwa wakikatwa
kodi hiyo moja kwa moja kutoka kwenye mishahara yao ambayo haikidhi mahitaji
ikilinganishwa na gharama za maisha ya kila siku.
No comments:
Post a Comment