Waziri wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid. |
Dkt. Rashidi alisema hayo jana wakati wa
kilele cha Siku ya Maadhimisho ya Mazingira Duniani yaliyofanyika jijini
Mwanza kitaifa, ambapo utafiti huo matokeo yake yanaonyesha kuwa ni
asilimia 29.6 hazina vyoo kabisa
huku asilimia 9 kuna vifaa maalum kwa ajili ya kunawa mikono jambo
ambalo ni hatari kubwa kwa afya kutokana na wananchi wengi kuwa na
mwitikio mdogo wa kujenga vyoo vya bora vya kisasa.
Hakuna matengenezo pale uharibifu unapotokea. |
Rashidi alisema pia Wizara hiyo ilizindua Kampeni ya kitaifa ya usafi na mazingia ya miaka minne iliyozinduliwa na mwaka
2012 iliyolenga kuwezesha kaya milioni 1,520,000 kupata huduma bora za
vyoo nchini ifikapo mwaka 2015 ambpo hadi sasa kampeni hiyo imefanikisha
kaya 312,528 kujenga vyoo bora sawa na asilima 56.4 ya lengo hilo.
Hakuna milango kwaajili ya kujisitiri, hakuna dawa wala usafi siyo suala la kuzingatiwa ni hali ya vyoo kwa baadhi ya shule zetu nchini. |
Choo si sehemu inayopewa kipaumbele na huchukuliwa kama sehemu chafu hivyo huwekwa mbali na makazi. |
Waziri
Dkt. Rashid alitangaza washindi wa tuzo za mashindano ya Afya na Usafi
wa Mazingira kwa mwaka 2014, kundi la kwanza lilihusisha Halmashauri za
Majiji manne ya Tanga, Mbeya, Mwanza na Dar esalam ambapo Jiji la Mwanza
limeibuka kuwa mshindi kwa asilimia 75 ikiwa ni mara ya tisa mfurulizo,
Halmashauri za Mikoa mshindi ni Manispaa ya Kinondoni ilibuka kwa
asilimia 55.7 kwa mshindi mmoja.
Kundi
jingine la tatu lilishirikisha Halmashauri za Manispaa 15 ambapo mshindi
wa kwanza ni Manispaa ya Iringa kwa asilimia71.3, mshindi wa pili
Manispaa ya Moshi kwa asilimia 68.1 na mshindi wa tatu ikichukuliwa na
Manispaa ya Morogoro kwa asilimia 67, kundi la nne ni Halmashauri za
Miji ambapo washindi asilimia zao kweny mabano kuwa ni Mji wa Njombe
(67.1), Kahama (63.2) na Mpanda (60.2).
Wito
wangu ni kuikumbusha jamii juu ya ungonjwa hatari wa Dengue ambao
umetokea mlipuko wa wagonjwa 1,119 kupatwa na kutokea vifo vya watu
wanne, kufatia kuumwa na mbu aina ya “Aedes” ambaye hupata mazalia
katika maeneo ambayo si safi akitolea mfano vifuu vya nazi , makopo,
vyungu vilivyotupwa hovyo, matairi ya magari na maji ya bafuni hivyo
kuwataka kuchukua hatua ya kuweka mazingira katika hali ya usafi.
No comments:
Post a Comment