MWILI WA MAREHEMU BENEDICT UKIONDOLEWA NA POLISI ENEO LA TUKIO
Polisi jijini Arusha wamedhibitisha kutokea kwa tukio la mauaji ya mtu mmoja ambaye ametambulika kwa majina ya BENEDICT GABRIEL umri miaka 58 mnafanya biashara wa madini na mkazi wa Moshono nje kidogo ya jiji la Arusha ,tukio ambalo lilitokea jana majira ya saa tatu na robo .
Tukio hilo la kusikitisha na lilizozua sintofahamu jijini Arusha lilitokea katika eneo la mtaa wa Maeda kati kati ya jiji la Arusha ambapo majambazi walitumia pikipiki aina ya toyo waliweza kusabisha kifo cha bwana Benedict kisha kuiba pesa za kitanzania 5,000,000/= kisha kutokomea pasipo julikana .
Tukio hilo la majambazi lilianzia kutoka Impala hotel ambapo mama mmoja aliyetambulika kwa majina ya Monica Msuya mkazi wa Mbauda jijini Arusha alikuwa ametoka kuchukua pesa hizo ,ambazo alikuwa maehifadhi kwenye mkoba wake .
Akiwa anaelekea kazini bi Monica alitumia usafiri wa tax na aliposhuka ili kufungua mlango wa ofisi yake alitokea kijana mmoja ambaye alimchapa vibao viwili na kukata ngwara kisha kuanguka chini ,lengo la kijana huyo ni chukua mkoba wa mama huyo .
Mama huyo alingangania mkoba wake na ndipo alipomua kupiga kelele za kuomba msaada huku akiwa maeshikilia kwa nguvu zote mkoba wake ili usichukuliwe na kijana yule,ndipo marehemu Benedict alipojitokeza kwa lengo la kumsaidia mama huyo ili asiibiwe mkoba wake.
Hapo ndipo kijana ambaye alikuwa amebaki na toyo alipotoa bunduki aina ya shotgun na kumlenga marehemu BENEDICT GABRIEL risasi ambayo ilisabisha kifo chake palepale,na ndipo kijana wa pili alipopata nafasi ya kuiba mkoba wenye pesa kisha kutokea pasipo julikana kwa kutumia pikipiki aina ya toyo yenye rangui nyekundu akiwa na mwenzake .
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi juu ya tukio ili kuweza kubaini watu waliohusika na tukio hilo huku mwili wa marehemu Benedict ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru.
Mipango ya mazishi ya marehemu Benedict inafanyika nyumbani kwake Moshono jijini Arusha na blog hii inatoak pole kwa familia ndugu jamaa na marafiki kwa msiba huu.
No comments:
Post a Comment