Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Maifa la Kuhudumia wakimbizi nchini, Joyce Mends Colc,akihutubia wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Nelson Mandela iliyofanyika jana, duniani kote na hapa nchini imeadhimishwa katika shule ya watoto wenye mahitaji maalum na kudhaminiwa na Vodacom.
Ofisa Habari wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini, Stella Vuzo,(kulia) akibadilishana mawazo na maofisa wa kampuni ya Vodacom, Matina Nkurlu na Gloria Mtui. Kushoto ni Ofisa wa Ubalozi wa Afrika ya Kusini, Nkhetheleni Mphohoni ,wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Nelson Mandela iliyofanyika jana, duniani kote na hapa nchini iliyoandaliwa na Ubalozi wa Afrika ya kusini nchini na kuadhimishwa katika shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Sinza, jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom wakishiriki katika kusafisha mazingira ya shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Sinza wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Mandela iliyofanyika jana na kuadhimishwa shuleni hapo iliyoandaliwa na ubalozi wa Afrika ya Kusini nchini kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
Ofisa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Gloria Mtui akishikiana na wanafunzi wanaosoma katika shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Sinza jijini Dar es Salam, kusafisha mazingira ya shule hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Mandela iliyoandaliwa na Ubalozi wa Afrika ya kusini nchini kwa ushirikiano wa Vodacom.
Baadhi
ya wanafunzi wa wanaosoma katika shule yenye mahitaji maalum ya Sinza
jijini Dar es Salam, wakiwa katika picha ya pamoja wakati
wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Nelson Mandela iliyoandaliwa na
Ubalozi wa Afrika ya kusini nchini kwa ushirikiano na Vodacom Tanzania.
WAFANYAKAZI
wa Ubalozi wa Afrika ya kusini nchini na baadhi ya wafanyakazi wa
kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania jana, Julai 18, 2014
wameungana na taasisi na wananchi kutoka sehemu mbalimbali duniani
katika kuadhimisha siku ya aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika
ya Kusini aliyejitolea maisha yake kupigania na kuondoa vitendo vya
ubaguzi wa rangi na unyanyasaji nchini humo,hayati Nelson Mandela.
Siku
ya Mandela ilitangazwa na Umoja wa Mataifa kuadhimishwa tarehe ya leo
kila mwaka na imekuwa ikiadhimishwa siku kama hii sehemu mbalimbali
duniani ambapo taasisi mbalimbali hushiriki kufanya kazi za kujitolea
kuhudumia jamii kwa muda wa dakika 67 kumuenzi kiongozi huyu aliyeleta
mapinduzi makubwa yenye historia ya kipekee duniani.
Katika
kuienzi siku hii ya leo,Ubalozi wa Afrika Kusini nchini ,Kituo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa, wafanyakazi wa kampuni ya simu za
mkononi ya Vodacom wameshiriki katika shughuli za kuhudumia jamii
ambapo wamesafisha mazingira ya shule ya watoto wenye mahitaji maalum
ya Sinza jijini Dar es Salaam ambapo pia wamegawa zawadi mbalimbali kwa
watoto wanaosoma shuleni hapo.
Kaimu
Balozi wa Afrika kusini nchini, Terry Govender alisema wanajivunia
kuwa na kiongozi hodari kama Nelson Mandela ambaye alijitolea nusu ya
maisha yake kupigana dhidi ya ubaguzi mchini Afrika Kusini na kuwaasa
watu kufwata nyayo zake kwani ni mfano wa kuigwa duniani.
“Kama
ilivyokuwa kwa Nelson Mandela, alitumia mda wake na nguvu zake
kuhamasisha amani na usawa na kupigania haki za wanyonge, Mandela pia
kupitia mfuko wa watoto aliouanzisha, aliamini kuwa watoto wote
wanapaswa kufurahia kukosekana kwa njaa, unyonyaji, unyanyasaji na
kutokuwa na makazi, hivyo ndio maana sisi tunashiriki kwa kuirudishia
jamii kile tulicho nacho na kufurahi pamoja na hawa watoto”, alisema.
Akiongea
juu ya kushiriki katika tukio hili muhimu,Meneja Uhusiano wa Umma wa
Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema kuwa kampuni inaona fahari kubwa
kushiriki na kutoa udhamini kwa tukio hili muhimu la siku ya kiongozi
mashuhuri duniani mwenye historia ya pekee katika mapambano ya
kutokomeza vitendo vya kufifisha haki za binadamu.
“Vodacom tunajivunia kushiriki katika shughuli za kijamii za kuadhimisha siku maalum ya kiongozi shupavu wa Afrika,hayati
Nelson
Mandela, aliyejitolea maisha yake yote kupambana na vitendo vya ubaguzi
wa rangi nchini Afrika na kuhakikisha vinatokomezwa kwa njia ya
amani”alisema Nkurlu.
Alisema
mbali na kumuenzi hayati Mandela kwa kutokomeza vitendo vya
ubaguzi,Vodacom inatambua mchango mkubwa wa kiongozi huyo alivyokuwa
mstari wa mbele kuhudumia jamii na moja ya sera ya kampuni ya Vodacom ni
kushiriki katika kazi za kuhudumia jamii.
“Kwetu
Vodacom kushiriki katika shughuli za kijamii ni moja ya sera yetu hivyo
siku hii ni muhimu kwetu kama kampuni na wafanyakazi wake wote na siku
zote tutakuwa mstari wa mbele kushiriki na kusaidia katika shughuli za
jamii.Alisema.
Hayati
Nelson Mandela ambaye alifariki mwaka jana desemba atakumbukwa daima
kwa ushupavu wake wa kutokemeza vitendo vya kibaguzi nchini Afrika ya
Kusini na baada ya kustaafu aliendelea kuisaidia changamoto mbalimbali
za kijamii kupitia taasisi ya Mandela Foundation.
No comments:
Post a Comment