Wananchi wa kata ya them, eneo la magorofa ya aicc
wamelalamikia ubovu wa barabara za ndani, kuzunguka magorofa hayo ,ambazo zina
zaidi ya miaka ya miaka 16 sasa bila ukarabati
wananchi hao wamelalamikia uongozi mzima unaosimamia
barabara hizo zinazoingia na kutoka katika nyumba hizo zinazomilikiwa na
taasisi kubwa, inayomiliki , ukumbi
mkubwa wa mikutano ya kimataifa na mashuhuri wa Aicc jijin Arusha.
Pamoja na ubovu wa barabara hizo ,tayari umejitokeza
usumbufu kwani magari ya mizigo yamekatazwa kupita katika barabara hizo ,eti
lengo ni kuhifadhi barabara hizo chakavu ziliyojaa mashimo kama mahandaki ,kwa
kuweka mageti na walinzi kila kona.
Walinzi hao nao,
wameanzisha mradi wao ,wa kujikusanyia shiling elfu moja moja, kutoka
kwa madereva wanaotaka kupita na magari yenye mizigo hata ile isiyozidi nusu
tani.
Wananchi na wakazi wa eneo hilo wamepania kufuatilia kwa
kina suala hilo,kwa uongozi ili kujua ufafanuzi na suluhusho la barabara hiyo, iliyotelekezwa
bila ungalizi.
Kutoka them jijin Arusha ni Gasper sambweti wa g sambweti
blog
No comments:
Post a Comment