Jumla
ya makundi kumi yamefanikiwa kuingia katika mchuano wa nusu fainali ya
shindano la Dance 100% shindano hilo linaloandaliwa na kituo cha (EATV)
chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Tanzania,yanaendelea kupamba moto ambapo hapo juzi hatua ya robo fainali
ilifanyika katika uwanja wa Don Bosco Mbuyuni Namanga jijini Dar es
Salaam na makundi 10 yalifanikiwa kuchukua tiketi ya kuingia nusu
fainali.
Mratibu
wa shindano hilo Happy Shame aliyataja makundi yaliyofanikiwa kuingia
nusu fainali kuwa ni Wazawa Crew,Best Boys Crew,G.O.P,The WT,Tatanisha
Dancers, Quality Boys, Wakali sisi, Mazabe Powder,The Winners Crew, Dar
Crew,
Mratibu wa mashindano hayo,Happy Shame,alisema kuwa amefuhishwa na
juhudi zinazofanywa na washiriki katika shindano hilo na anawapa pongezi
sana majaji kwa kuwa makini na kuweza kupata makundi 10 rasmi
yaliyoingia moja kwa moja ngazi ya nusu fainali.
“Huu
ni mwaka wa tatu East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya kwa
udhamini wa Vodacom Tanzania na Mwaka huu tumeungwa mkono na Grand Malt
kama kinywaji rasmi cha Dance 100%. Kwa kweli nitakuwa mchoyo wa fadhila
kama sitaweza kutoa shukururani zangu kwa wadhamini kwani wasingekuwa
wao tusingekuwa hapa tulipo”Alisema Happy.
Happy,
aliongeza kwamba kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya
ambayo pia yamekuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha EATV kila
jumatano saa moja kamili usiku,litajishindia kitita cha shilingi
milioni 5.
Naye
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa
mashindano haya,Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom inatoa udhamini kwa
kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambayo yanaweza kutoa ajira
sahihi kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.
Alisema
kuwa kwa niaba ya Vodacom Tanzania,anayapongeza sana makundi hayo 10
yaliyoingia nusu fainali na kwa kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la
ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote
ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi basi wanajisikia fahari
sana kwa vijana hao kuingia nusu fainali ndio maana siku zote Vodacom
imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na
tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani.
“Vodacom
tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta
mbalimbali iwapo watawezeshwa hivyo tunadhamini mashindano haya
tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na
kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia
katika sanaa”Anasema Nkurlu.
Alisema
jinsi siku zinavyoenda ndiyo jinsi anavyowaona vijana wanaoshiriki
katika shindano hilo wamekuwa makini kwa kile wanachokifanya kwani
wametambua kuwa michezo ni ajira na wanaitumia fursa hii waliyoipata
ipasavyo ili waweze kujikomboa kiuchumi “Suala la ajira kwa vijana sio
lazima kufanya kazi viwandani au maofisini tu bali kuna njia nyingi za
kujiajiri na kujipatia kipato mojawapo ikiwa ni kupitia michezo,muziki
na sanaa nyingine na Vodacom siku zote tupo mstari wa mbele kuinua
vipaji vya vijana na kuweza kujikwamua kiuchumi”Alisisitiza Nkurlu.
Kikundi
cha Quality Boys cha Kinondoni jijini Dar es salaam, kikionyesha
umahiri wao wa wakati wa robo fainali ya shindano la Dance100%
lililofanyika katika Viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es
Salaam .Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom
Tanzania mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi
milioni 5.
Vijana
wa kundi la Tamtamu la Ilala jijini Dar es salaam, wakikonga nyoyo za
mashabiki kwenye robo fainali ya shindano la Dance 100% linaloandaliwa
na EATV na kudhamiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Viwanja vya
Don Bosco Oysterbay.Kundi litakaloshinda litajinyakulia kitita cha
shilingi milioni 5.
Kundi
la Dar Crew la Mbagala jijini Dar es salaam, wakishiriki robo fainali
ya shindano la Dance100% lililofanyika kwenye Viwanja vya Don Bosco
Oysterbay .Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom
Tanzania.Mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi
milioni 5.
Umati
wa watu waliofurika kwenye Viwanja vya Don Bosco Oysterbay Dar es
Salaam, wakifuatilia mchuano wa robo fainali ya shindano la Dance100%
lililoandaliwa na EATV na Kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Kundi
la W.T la Temeke la jijini Dar es Salaam,wakikonga nyoyo za mashabiki
wakati wa robo fainali ya Shindano la Dance% lilifanyika kwenye viwanja
vya Don Bosco Oysterbay.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na
kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Kikundi
cha T.O.P cha Temeke jijini Dar es Salaam,wakiburudisha vilivyo wakati
wa robo fainali ya Shindano la Dance% lililofanyika kwenye viwanja vya
Don Bosco Oysterbay.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na
Vodacom Tanzania.Mshindi ataondoka na kitita cha shilingi Milion 5.
No comments:
Post a Comment