Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya D’Salaam limewashauri albino wanaoishi Jijini D’Salaam kuwa karibu
sana na Jeshi hilo ili kurahisisha mawasiliano kati yao na Wakuu wa vituo vya
Polisi vilivyo karibu na makazi yao au wanapofanyia usalama wao jijini
D’Salaam.
Pamoja na kwamba
haijawahi kutoa tukio lolote dhidi ya Albino jijini D’Salaam kutokana na
uhusiano uliopo lakini kwa sasa waongeze mawasiliano na Jeshi la Polisi kutokana
na taarifa za uhalifu dhidi ya Albino katika baadhi ya mikoa hapa nchini. Pia Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi
D’Salaam SULEIMAN KOVA ameongea na Albino hao ofisini kwake na kuwaambia kwamba
Jeshi la Polisi kwa ujumla linaendelea na jitihada kubwa sana kupambana na
maadui wa Albino ambao ni wahalifu na wengi wao wameishakamatwa na kufikishwa
mahakamani ambapo wengine wameishahukumiwa.
Albino wanatakiwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na Jeshi la Polisi
hata kama hakuna tishio la aina yoyote wanalolijua katika maeneo yao ya makazi
au wanapofanya shughuli zao za kikazi.
Katika kufanikisha
zoezi hilo la mawasiliano ya haraka na Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi
Kanda Malum ya D’Salaam kwa kushirikiana na wadau kampuni ya SAPNA ELECTRONIC ametoa
simu 20 kwa Albino ambao wameudhuria kikao ili iwe rahisi kwao kuwasiliana
Jeshi la Polisi kwa namba 0787-668306 ambayo ipo katika chumba cha dharura
katika Kikosi cha 999. Kamishna Kova
anaendelea kuongea na wadau mbali mbali ili misaada zaidi ipatikane kwa
walemavu wa ngozi ambao ni Albino ili waweze kupata simu za mikononi, mafuta
maalum ya kupaka ngozi zao na msaada mwingine wowote ambao utafaa kwa Albino
hao kupitia kwa namba 0715 – 009983 hii ni namba ya Kamishna mwenyewe ya oisi
na namba nyingine ya Msaidizi wake katika suala la kuwasaidia Albino ni
0756-710179 ambayo ni ya SP. MOSES NECKEMIAH FUNDI.
Aidha zipo jitihada za makusudi
zinazofanyika kati ya Polisi Kanda Maalum ya Polisi D’Salaam na uongozi wa Mkoa
na Kitaifa kwa manufaaa ya ulinzi na Usalama wa Albino wote.
Hatua zingine za ziada za muda mfupi
na mrefu ni uwepo wa program ya mafunzo maalum kwa Albino wa Jijini D’Salaam
ili wapate mafunzo kupitia dhana ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kwa lengo
la kupata uelewa wwa kutosha ili nao pia washiriki na kujua namna ya kutoa
taarifa kwa lengo la kujikinga na maadui wao ambao wamegubikwa na tama za
kujipatia mali, madaraka n.k. kwa njia za ushirikina.
No comments:
Post a Comment