Mmoja
wa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza
Mori,jijini Dar es salaam akionyesha umahiri wake wa kudaka taswirazz
kwa kutumia simu.
Afisa
Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Amne Hilal akipata
Selfie na baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye kituo cha CHAKUWAMA
kilichopo Sinza Mori,jijini Dar es salaam,wakati walipowatembelea leo
kusherehekea nao kuukaribisha mwaka mpya wa 2015.
Afisa
Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Amne Hilal akiwaonyesha
picha yao watoto hao wanaolelewa kwenye kituo cha CHAKUWAMA kilichopo
Sinza Mori,jijini Dar es salaam
Mmoja wa watoto waliopo kwenye kituo hiyo.
Mmoja
wa maafisha wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Lusajo Mwakabuku
akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa Shirika
la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan Mhaiki (mwenye shati jeupe
walioketi mbele) wakati walipowatembelea na kusherehekea nao mwaka mpya
2015,watoto wanaolelewa kwenye kituo cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza
Mori,jijini Dar es salaam.
Katibu
Mtendaji wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,Hassan Hamis
(aliesimama) akitoa maelezo mafupi kuhusu kituo hicho mbele ya uongozi
wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) waliotembelea kituo hicho kwa
lengo la kujumuika pamoja na watoto hao katika kusherehekea kuukaribisha
mwaka mpya wa 2015.
Afisa
Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Leila Muhaji akifafanua
jambo mbele Watoto Yatima wanaolelewa kwenye kituo cha CHAKUWAMA
kilichopo Sinza Mori,jijini Dar es salaam.
Katibu
Mtendaji wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,Hassan Hamis
(kulia) akitoa maelezo ya kituo hicho kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la
Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan Mhaiki wakati alipokuwa
akimtembeza kwenye maeneo mbali mbali ya Kituo hicho.Kushoto ni Afisa
Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Leila Muhaji.
Katibu
Mtendaji wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,Hassan Hamis
akifafanua jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco),Mhandisi Decklan Mhaiki wakati wakiwa kwenye moja chumba cha
msimamizi wa kituo hicho ambacho kipo katika hatua za mwisho kumalizika.
Amne Hilal akifurahi na Baadhi ya Watoto wa kituo hicho.
Mlezi
Mkuu wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,Bibi Saida Hassan
akizungumza na vyombo vya habari wakati uongozi wa Tanesco ulipotembelea
kituo chake hicho.
Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan
Mhaiki akizungumza na wanahabari mara baada ya kutembelea maeneo mbali
mbali ya kituo hicho,ambapo amefarijika sana kuona maendeleo ya watoto
katika kituo hicho.ambapo waliweza kuwapatia watoto hao vifaa vya shule
na vyakula kama sehemu ya mchango wao.
Katibu
Mtendaji wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,Hassan Hamis
akitoa shukrani kwa uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa
kuwatembelea kituoni hapo,huku akitoa wito kwa wengine kuendelea
kukitupia macho kituo hicho,kwani bado kinahitaji kusaidiwa.
Afisa
wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Khadija Ahmed (kati) akimnyesha
maziwa Mtoto Badra mwenye umri wa miezi saba (7) anayelelewa kwenye
kituo hicho baada ya kutupwa na Mama yake nje ya kituo hicho akiwa na
miezi mitano (5).wanaoshuhudua ni Queen Mwashinga (kulia) na Henry
Kilasila.
Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan
Mhaiki akimkabidhi baadhi ya vifaa mmoja wa watoto wanaolelewa kwenye
kituo hicho ikiwa ni sehemu vifaa walivyowaletea watoto hao.
Sabuni.
Sehemu ya vifaa vilivyotolewa na Tanesco kwa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA.
Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan
Mhaiki akimkabidhi risiti ya Umeme Katibu Mtendaji wa Kituo cha kulea
Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,Hassan Hamis ikiwa ni moja ya vitu
vilivyokuwa vikihitajika kituoni hapo.
Maafisa wa Tanesco,Neema Mbuja (kulia) na Amne Hilal wakiweka mambo sawa kabla ya kukabidhi kwa uongozi wa kituo hicho.
Muda wa chakula ukawadai.
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment