Mkurugenzi
Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles akiongea na waandishi wa
habari(hawapo pichani) wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni ya Tigo
kwa wanariadha ambao walishinda mbio za mwaka jana za Tigo Ngorongoro
Run Marathon kushirki kwenye mbio za mwaka huu za Tigo Kili Half
Marathon, Kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha
na Kulia kwake ni mwanariadha Mary Naali na Mjumbe toka Riadha Tanzania
Meta Petro. Mkutano huo ulifanyika Mkoani Arusha jana.
Mwanariadha
Alphonce Felix akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati
kampuni ya Tigo ilipotangaza udhamini kwa wanariadha ambao walishinda
mbio za mwaka jana za Tigo Ngorongoro Run Marathon kushirki kwenye mbio
za mwaka huu za Tigo Kili Half Marathon. Pembeni kulia ni .Mkurugenzi
Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles na Meneja wa Mawasiliano
wa Tigo John Wanyancha.
Mwanariadha
Mary Naali akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati
kampuni ya Tigo ilipotangaza udhamini kwa wanariadha ambao walishinda
mbio za mwaka jana za Tigo Ngorongoro Run Marathon kushirki kwenye mbio
za mwaka huu za Tigo Kili Half Marathon. Pembeni kulia ni .Mkurugenzi
Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles na Meneja wa Mawasiliano
wa Tigo John Wanyancha na kushoto ni Meta Petro Mjumbe toka riadha
Tanzania pia ni kocha wa wanariadha hao.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles akipeana mkono na
Alphonce Felix mara baada kutangaza udhamini wa Kampuni ya Tigo kwa
wanariadha walioshinda mbio za Tigo Ngorongoro Run Marathon mwaka jana
waweze kushiriki mbio za mwaka huu za Tigo Kili Half Marathon
zitakazofanyika tarehe 1 machi Moshi Mkoani Kilimanjaro. Pembeni
anayeshuhudia ni Mwanariadha Mary Naali.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles (nyuma katikati) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wanariadha walioshinda mbio za Tigo Ngorongoro
Run Marathon mwaka jana mara baada ya kutangaza udhamini wa Kampuni ya
Tigo kwa wanariadha hao kushiriki mbio za mwaka huu za Tigo Kili Half
Marathon zitakazofanyika tarehe 1 machi Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Pembeni kulia mstari wa nyuma ni John Wanyancha Meneja wa Mawasiliano wa
Tigo.
No comments:
Post a Comment