Mbunge Dkt. Raphael Chegeni
Na Tiganya Vincent-MAELEZO_Dodoma
BAADHI
ya Wabunge wanaotoka Kanda ya Ziwa wameomba Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi
na Mawasiliano kujenga Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa kiwango cha
Kimataifa ili kuimarisha sekta ya Utalii na usafiri wa anga katika kanda
ya Ziwa.
Walisema
kuwa hatua itasaidia watalii wanaokuja nchini kushuka moja kwa moja
mkoani Mwanza na kisha kuelekea katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na
maeneo mengine ya vivutio vya hapa nchini bila kupitia nchi jirani.
Kauli hiyo imetolewa jana na Wabunge Dkt. Raphael Chegeni na Mhe. Ezekiel Maige wakati wakichangia hotuba kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka ujao wa fedha.
Mhe.
Dkt.Chegeni alisema kuwa Uwanja wa Ndege wa Mwanza ni muhimu ukajengwa
kwa viwango vya Kimataifa ili uweze kuruhusu ndege mbalimbali kubwa na
ndogo kuweza kutua bila tatizo.
Alisema
kuwa hatua hiyo itasaidia kuunganisha Mkoa wa Mwanza na nchi jirani za
Rwanda, Uganda na Burundi na hivyo kuruhusu ndege nyingi kutoka Nchi
hizo kutua bila kwenda katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere .
Mhe. Dkt. Chegeni aliongeza
kuwa uwanja huo endapo utajengwa kwa kiwango cha Kimataifa utasaidia
kuwa kiungo muhimu kwa mikoa 10 ya kanda ya ziwanana kati.
Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Ezekiel Maige
Naye
Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Maige alisema kuwa ujenzi wa Uwanja wa
Ndege wa Mwanza sio tu utasaidia kuunganisha mkoa huo na mikoa mingine
bali utasaidia kuchochea uchumi
wa eneo la Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla kwani watalii na
wasafiri wengine watakuwa na fursa ya kuingia Mwanza bila kupitia nchi
jirani.
Aliongeza
kuwa endapo zoezi hilo litafanyika kwa kiwango cha kimataifa litatoa
fursa kwa ndege nyingi za ukumbwa tofauti tofauti kutua katika Uwanja
huo na hivyo kupunguzia wananchi ughali wa bei unaotozwa na baadhi ya
Kampuni za Ndege ambazo zinatoa huduma za usafiri mkoani humo.
No comments:
Post a Comment