Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali iliamua kununua
ndege aina ya Bombadier Q400 kutoka Canada kutokana na
uhitaji wa huduma ya usafiri wa anga kwa safari za ndani ya
nchi na mazingira halisi ya viwanja vya ndege vilivyopo nchini.
Profesa Mbarawa alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua
mafunzo ya wakufunzi ya marubani yanatolewa na Chuo cha
Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Mabibo, Dar es Salaam.
“Serikali imeamua kununua aina hii ya ndege za Bombadier
Q400 kutokana na hali halisi ya viwanja vya ndege nchini kuwa
vya changarawe na lami kwa baadhi,” alisema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa aliyeonekana kujibu hoja za wabunge wa
Kamati ya Miundombinu walipokutana na Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) mjini
Dodoma hivi karibuni, alisema kuwa Serikali haikukurupuka
kufanya uamuzi wa kununua aina hiyo ya ndege kwani
ilizingatia vigezo na malengo mahsusi ya kuhudumia usafiri wa
ndani na kuboresha usafiri wa anga kupitia ATCL.
Katika kikao hicho cha Kamati ya Bunge ya Miundombinu,
Mbunge wa Misungwi (CCM) na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya
Ndani, Charles Kitwanga alipinga Serikali kununua ndege hizo
zinazotumia injini za pangaboi kwa fedha taslimu huku kukiwa
hakuna mipango thabiti ya kuifanya ATCL iwe bora.
“Ukiangalia mikakati ya kutanua hili shirika (ATCL) liende juu
hakuna, tunachozungumzia ni kununua ndege. Sasa ukishanunua
zije zifanye nini? Zife na zenyewe? Ziishe kama tulivyonunua
nyingine? Hivyo ndivyo tutakavyoendesha uchumi wetu, mimi
naambiwa Q400 ndiyo tutakuwa watu wa kwanza kuipokea,
halafu mnaifahamu hii kampuni? Si kubwa kama inavyotajwa, ni
mali ya mtu binafsi,” alisema.
Lakini Profesa Mbarawa alitetea uamuzi wa kununua ndege hizo
huku akiwataka Watanzania kuelewa nia ya Serikali yao ni
kuhudumia wananchi, hivyo watu wasipotoshe ukweli kuhusu
ndege hizo kwa kuwa zimezingatia mambo mbalimbali likiwamo
suala la usalama na ufanisi katika uendeshaji wake.
Uwezo na ubora
Profesa Mbarawa alisema ndege hizo zina uwezo wa kutua katika
viwanja vingi vyenye urefu wa kilomita 1.5 ambavyo ni vingi
nchini tofauti na aina nyingine ambazo hutua kwenye viwanja
vyenye urefu zaidi ya kilomita mbili.
Pia, zinatumia kiasi kidogo cha mafuta ikilinganishwa na aina
nyingine ambapo kwa safari ya kutoka Dar es Salaam hadi
Mwanza zitakuwa zikitumia tani 1.7 za mafuta tofauti na aina
nyingine zinazotumia hadi tani 2.8 kwa safari moja.
Vilevile, alitumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulionezwa kuwa
ndege hizo zimenunuliwa katika kampuni ndogo isiyokuwa na
sifa akisema kampuni hiyo imefanya biashara na nchi nyingi
ikiwamo Ethiopia yenye ndege 19 aina ya Bombadier Q400
zilizotengezwa na kampuni hiyo.
Tayari Serikali imeshafanya malipo ya ununuzi wa ndege hizo
kwa asilimia 40 na zitaanza safari ya kutoka Canada Septemba
15 mwaka huu kupitia Uingereza na zinatarajiwa kuwasili nchini
Septemba 19.Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,

Septemba 19
No comments:
Post a Comment