Tuesday, August 23, 2016

Taarifa za kwanza kuhusu mauaji ya Polisi Dar usiku huu

Moja ya stori zinazosambaa kupitia mitandao ya kijamii usiku huu wa August 23 2016 ni pamoja na hii inayodaiwa kuuawa kwa askari polisi wawili kufuatia tukio la uporaji lililotokea katika bank ya CRDB tawi la Mbande, Mbagala.
Millardayo.com imemtafuta kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro ambaye amesema…>>’Ni kweli kumetokea tukio la uvamizi hapa mbagala lakini kwa taarifa kamili ntazitoa kesho kwakuwa bado nipo eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi
Endelea kukaa karibu na millardayo.com kwa ajili ya kukusogezea taarifa kamili itakayonifikia kwakuwa tayari ripota wangu yupo njiani kuelekea eneo la tukio.
ULIIKOSA HII KAMANDA SIMON SIRRO KUHUSU ‘UKUTA’


No comments:

Post a Comment