Ametoa agizo hilo mjini Arusha alipoahirisha kesi zinazomkabili Mbunge huyo anayetuhumiwa kusambaza ujumbe unaomkashifu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kuhamasisha wananchi kufanya maandamano Septemba Mosi, mwaka huu.
“Kuna maelekezo yametolewa baadhi ya kesi watu wa mashitaka mnatakiwa kuzileta mahakamani kabla hamjakamilisha upelelezi. Lakini pia kuna kesi kama hizi zilizopo mbele yetu mnatakiwa kuzileta mkiwa tayari mmekamilisha upelelezi,”alisema Rwizile bila kufafanua.
Agizo hilo la hakimu limetolewa baada ya upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Jamhuri, Blandina Msawa kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo ulikuwa haujakamilika na hivyo kuomba tarehe nyingine.
Hakimu Rwizile aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 12 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Vilevile aliuagiza upande huo wa mashitaka kukamilisha upelelezi ili mtuhumiwa asomewe hoja za awali za mashitaka yanayomkabili.
Katika kesi hiyo, Lema anawakilishwa na Wakili, John Mallya na jana mtuhumiwa huyo hakuweza kufika mahakamani kutokana na wadhamini wake kusema kuwa yuko katika kikao cha Bunge Dodoma.
Pamoja na kutolewa kwa udhuru huo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Rwizile aliuagiza upande wa utetezi kuhakikisha mtuhumiwa huyo anafika
mahakamani tarehe iliyopangwa asomewa hoja za awali za mashitaka yanayomkabili.
Inadaiwa kuwa kati ya Agosti 20, mwaka huu ndani ya Arusha, mtuhumiwa huyo alituma ujumbe kutoka namba 0764150747 kwenda namba 0766-757575 uliokuwa ukidai, “Karibu, tutakudhibiti kama Uarabuni wanavyodhibiti mashoga.”
No comments:
Post a Comment