Friday, June 8, 2012

Marekani kumzawadia atakayesaidia kukamatwa muasisi wa Al-shabab

 Marekani imetangaza kitita cha dola milioni 7 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazoisaidia kumkamata kiongozi namba moja wa kundi la Al-shabab la Somalia.
Mahmud Godane anayejulikana pia kwa jina la Abu Zubayr anakuwa mwanachama wa kwanza kutafutwa na Marekani kupitia njia hiyo. Huku hayo yakijiri, mapigano makali kati ya jeshi la serikali ya mpito ya Somalia na wapiganaji wa Al-shabab yameripotiwa viungani mwa mji wa bandarini wa Kismayu. Hii ni katika hali ambayo majuma kadhaa yaliyopita majeshi ya serikali yalifanikiwa kuchukua udhibiti wa mji muhimu na wa kistratejia wa Afmadow karibu na Kismayu kutoka mikononi mwa wanamgambo hao. Al-Shabab walianzisha vita dhidi ya serikali ya mpito ya Somalia mwezi Mei mwaka 2009 kwa lengo la kuiondoa madarakani.

No comments:

Post a Comment