Burudani nayo ilikua sehemu ya
kunogesha Nyerere Day
Ofisi
ya Mkuu wa Wilaya ya
Arusha kwa kushirikiana na wadau wa michezo pamoja na wananchi wa Jiji
wameadhimisha siku ya Mwl. Nyerere kwa kuandaa na kushiriki kwenye Bonanza la
Michezo lililopewa Jina la Bonaza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye
uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini hapa leo tarehe
14.10.2016.
Tamasha hili limeandaliwa
maalumu kwa ajili ya kumuenzi baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyenyere
aliyefariki miaka kumi na saba iliyopita sambamba na kusherekea kilele cha
Mwenge wa Uhuru ambao ulipita katika Wilaya ya Arusha mwishoni mwa mwezi wa nane
na kuzindua miradi ya Afya, Maji, Elimu, Uwezeshaji wananchi, uwezeshaji
makundi maalumu, Ujenzi na Usafi wa Mazingira yenye thamani ya zaidi ya TshBil
1.5.
Akiongea na wanamichezo
walioshiriki katika Bonanza hilo Mkuu wa Wilaya ya Arusa Mhe. Gabriel Fabian
Daqarro alisema Tamasha hili ni kwa ajili ya kumuezi Mwl. Nyenyere ambapo
litasaidia vijana na wananchi kuweka miili yao safi, kujiepusha na maradhi
pamoja na makundi yanayoweza kusababisha kujiingiza kwenye madawa ya kulevya,
ulevi na uzururaji.
Pia tuitumie siku hii
kutafakari mafundisho na maelekezo ya Mwalimu Nyerere aliyoyatoa wakati wa uhai
wake, wapi Nchi imetoka, Misingi imara ya Uongozi bora na namna gani tunaweza
kuenenda ili kuleta maendeleo katika Taifa letu, na vijana kama nyie ndio
mnaotakiwa kuwa chachu katika kupambana na umasikini katika Nchi yetu alisema
Dc Daqarro.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya
ya Arusha Bw. David Mwakiposa alielezea Tamasha hilo kuwa
limeshirikisha michezo mbalimbali kama Netball, Football, Volleyball,
Basketball, mchezo wa Bao, kukimbiza kuku, Baiskel, kuvuta kamba, Karate,
Taekondo, Uchoraji pamoja na riadha.
Bonaza hili pia limetumika
kama jukwaa la kuendelea kuelimisha na kueneza ujumbe kwa vijana kupitia kauli
mbiu ya Mwenge mwaka 2016 inayosema “Vijana ni nguvu kazi ya Taifa
washirikishwe na wawezeshwe”.
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari,
Halmashauri ya Jiji la Arusha
14.10.2016
|
No comments:
Post a Comment