Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akizungumza na washiriki wa mafunzo na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi uliofanyika leo katika chuo hicho kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akizungumza na washiriki wa mafunzo na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi uliofanyika leo katika chuo hicho kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Frank Mkumbo akizungumza na washiriki wa mafunzo na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi uliofanyika leo katika chuo hicho kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo uliofanyika leo katika chuo hicho kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Na Albert Fen, Dar es Salaam
24 Oktoba, 2016.
MKUU wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika(EASTC) Prof. Innocent
Ngalinda amezindua mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi ambayo yalianza
tarehe 17 Oktoba mwaka huu chuoni Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo
wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Prof. Ngalinda amesema mafunzo
hayo yameandaliwa kwa nia ya kumpatia mshiriki ujuzi katika ukusanyaji takwimu
kwa ajili ya kuzichakata na kuwa takwimu rasmi.
“Washiriki hawa
watafundishwa mbinu shirikishi, utatuzi wa matatizo mbalimbali wakati wa
ukusanyaji takwimu, sensa na viwango vya tafiti mbalimbali, utunzaji wa Vifaa
vya ukusanyaji takwimu kama vile simu za mkononi na kumpyuta mpakato
pamoja na kubadilisha madodoso ya kawaida na kuwa ya kisasa”, amesema Prof.
Ngalinda.
Akizungumzia
malengo ya mafunzo hayo Naibu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa
Kitaalamu wa chuoni hapo Dkt. Frank Mkumbo amesema lengo ni kuwawezesha
wakusanyaji takwimu kukusanya takwimu halisi na zenye ubora kwa ajili ya
kupanga mipango mbalimbali ya Maendeleo.
“Lengo kuu la mafunzo haya ni kuhakikisha kuwa wakusanyaji takwimu
rasmi wanakuwa na weledi wa kutosha katika kukusanya takwimu bora na zenyetija
kwa taifa” amefafanua Dkt. Mkumbo.
Jumla ya washiriki 110 wamejiunganamafunzohayomaalumu ya muda wa
miezimiwilikwa awamu ya kwanza ambayo yatamalizika mwezi Disemba, 2016 na
watakaomaliza na kufaulu watapatiwa cheti cha Ukusanyaji Takwimu. Awamu ya pili
ya mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza Novemba mwaka huu na kumalizika Januari,
2017.
No comments:
Post a Comment