Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse (kushoto), akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo
kuanza kutumia ndege mpya aina ya Embraer 190 kusafirisha abiria. Kulia
ni Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro.
Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse (katikati), akisisitiza jambo
kwenye mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Huduma kwa Wateja,
Christina Kausan.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
WANANCHI
wametakiwa kuchangamkia usafiri wa ndege wa Kampuni ya Fast jet baada
ya kampuni hiyo kuanza kutumia ndege mpya aina ya Embraer 190 ambayo ni
nafuu zaidi kwa matumizi.
Mwito
huo umetolewa na Dar es Salaam leo na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast
jet, John Corse wakati akizungumza na waandishi wa habari jana kuwa
ndege hizo ni rahisi kwa matumizi ya usafiri hapa nchini.
Alisema
kuwa ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 108 aliongeza kuwa
zitahudumia kwa miezi 6 huku ikitoa nafasi kwa mafunzo wa marubani wa
Fast jet hapa nchini.
Aliongeza
kuwa kwa kuwa Fast jet hapa nchini imepata hasara kiuendeshaji hivyo
ndege hizo kwa kuwa hazitumii matufa mengi itasaidia kuiimarisha
biashara.
"
Hii imetokea tu kuwa wakati serikali imeleta aina ya ndege zisizotumia
mafuta mengi na sisi tulikuwa pia tumeshaanza mchakato huo na hivyo kwa
sasa binafsi naona kuwa watanzania watanufaika zaidi" alisema Corse.
Pia
aliipongeza serikali kwa kuleta ndege mpya aina ya Bombardier 8, Q400
ambazo zinaenda mikoa ya Rukwa, Mara, Kagera na Dodoma ambapo ndege za
Fast jet hazifiki.
Alisema
kwa kuwa lengo la Fast jet ni kuwapatia watanzania huduma nafuu za
usafiri wa anga hivyo inafurahia pale ambapo inaona kuwa ndege za
serikali zinafika mikoa ambayo Fast jet haifiki.
No comments:
Post a Comment