Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (kulia)
akimkaribisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge
(kulia) alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Bukoba kujionea uharibifu
wa miundombinu ya sekta ya maji iliyosathiriwa na tetemeko la ardhi.
Katibu
Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kagera Mhandisi Avitus Exavery akimuonesha
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge uharibifu wa tanki
la maji la shule ya sekondari ya Ihungo uliosababishwa na tetemeko la
ardhi lililotokea mkoani Kagera mapema Septemba 2016.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge (wa nne kulia)
akitembelea miundombinu ya maji iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi
lililotokea mkoani Kagera mapema Septemba 2016.
Baadhi maungio ya maji yaliyoharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mapema Septemba 2016.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge (kulia) akiagana na Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (kulia) leo mjini
Bukoba kujionea uharibifu wa miundombinu ya sekta ya maji iliyosathiriwa
na tetemeko la ardhi.
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.
Serikali
imeanza kurekebisha miundombinu ya maji iliyoharibiwa na tetemeko la
ardhi mkoani Kagera ili kuwapatia wananchi huduma ya maji safi na salama
waweze kuendelea na kazi zao za kawaida za kila siku.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson
Lwenge alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum
Kijuu ofisini kwake leo mjini Bukoba kujionea uharibifu wa miundombinu
ya sekta ya maji iliyosathiriwa na tetemeko la ardhi.
“Ni
lazima turudishe miundombinu ya maji ambayo imeharibiwa na tetemeko la
ardhi ili kuwapatia wananchi huduma ya maji safi na salama, maji
wanaweza kuyapata lakini yanaweza kuwa si salama, ni kukumu langu kuja
kupita ili niweze kukagua kujua baada ya tetemeko hili bado maji ni
salama au kuna mambo ya kufanya ili tuweze kuyashughulikia” alisema
Waziri Mhandisi Lwenge.
Katika
kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Kagera wanapata maji ya uhakika, Waziri
Mhandisi Lwenge amesema kuwa ziara yake inalenga pia kuhakikisha azma
ya Serikali ya kuwapatia wananchi maji ya uhakika.
Mpango
huo wa Serikali unalenga kuwapatia wananchi waishio mijini maji kwa
kiwango cha asilimia 95 ambapo kwa wananchi waishio vijijini wanapata
maji ya uhakika kwa asilimia 85 ifikapo 2020.
Kwa
wananchi waishio vijijini, Waziri Mhandisi Lwenge amesema kuwa kwa sasa
wananchi wanapata maji kwa asilimia 60 hadi 70 wakati kwa ngazi ya
kitaifa inaonesha wananchi hao wanapata maji kwa asilimia 72.
Kwa upande wa sekta ya umwagiliaji, Waziri Mhandisi Lwenge amesema kuwa hali ya mvua nchni inazidi kupungua mwaka hadi mwaka.
Waziri
Mhandisi Lwenge amesema kuwa ili kuwa na uhakika wa chakula cha
kutosha, Serikali pamoja na wananchi kuweka nguvu kwenye kilimo cha
umwagiliaji ambacho ndio chenye uhakika wa kutatua changamoto ya uhaba
wa chakula na upatikanaji wa maji.
Katika
kukabiliana na hali hiyo, Waziri Mhandisi Lwenge amsema kuwa Serikali
imeanzisha Tume ya Umwagiliaji na kuainisha maeneo yanayofaa kwa kilimo
cha umwagiliaji ikiwemo mkoa wa Kagera ambayo yanaweza kutumika kwa
kilimo cha umwagiliaji.
Hatua
hiyo ya Serikali itasaidia kujengwa kwa miundombinu ambayo itawasidia
wananchi wanaoishi katika maeneo ya umwagiliaji waweze kufaidika kwa
kilimo cha umwagiliaji ambayo ndio azma ya Serikali.
Waziri
Mhandisi Lwenge amesema kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha ifikapo
mwaka 2020 kuwa na hekta milioni 1 za kilimo cha umwagiliaji ambapo kwa
sasa zinalimwa hekta 461,0000 ambayo ni sawa na asilimia 1.6 ya eneo
lote ambalo linaweza kutumika kwa umwagiliaji na kuutaja mkoa Kagera ni
moja wapo ya maeneo ambayo yanafaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
Zaidi
ya hayo, Waziri Mhandisi Lwenge amesema kuwa kulingana na jiografia ya
mkoa wa Kagera, upo uwezekano wa kujenga mabwawa ambayo yatatumika kwa
kilimo cha umwagiliaji, kufuga samaki, maji ya kunyweshea mifugo na
kuweka rasilimali maji ambayo nchi nyingi duniani zimeanza kutegemea
kilimo hicho ili kujihami na upungufu wa mvua.
Akimkaribisha
Waziri Mhandisi Lwenge, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu
Salum Kijuu amesema kuwa katika sekta ya maji mkoani humo, miundombinu
ya maji imeathirika na kuharibiwa na tetemeko la ardhi na kusababisha
upatikanaji wa maji kwa wananchi kuwa si wa kuridhisha.
Aidha,
Mkuu huyo wa mkoa amemhakikishia Waziri wa maji na umwagiliaji kuwa
maagizo na maelekezo yake aliyoyatoa yatasimamiwa na kutekelezwa ili
kuwahudumia wananchi na maisha yao yaweze kuwa bora na kujiletea
maendeleo.
Katika
ziara yake mkoani Kagera, Waziri Lwenge ametembelea maeneo miundombinu
ya maji yaliyoharibiwa na tetemeko la ardhi, Mamlaka ya Maji Safi na
Salama Bukoba, chanzo cha maji cha Bunena pamoja na tanki la maji la
shule ya sekondari Ihungo lililoathiriwa tetemeko la ardhi.
No comments:
Post a Comment