Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibari (ZMA) Abdallah Hussein Kombo akizungumza
na waandishi wa Habari kukanusha tuhuma za kusajili Meli za Korea ya
Kaskazini kinyume na Azimio la Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa
Baharini Abdallah Hussein Kombo wakati
alipokutana nao Ofisini kwake Malindi .
Mwandishi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ramadhan Ali akimuliza suala
Mkurugenzi Mkuu (ZMA) hayupo pichani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar
Mustafa Aboud Jumbe akitowa ufafanuzi wa masuala yaliyoulizwa na Waandishi wa Habari
katika Mkutano huo. (Picha na
Miza Othman Habari Maelezo Zanzibar).
Na Ramadhan Ali/Maelezo Zanzibar 11.10.2016
Mamlaka
ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA) imekanusha tuhuma zinazotolewa
kuwa imesajili meli za Korea Kaskazini kinyume na Azimio la Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwezi Machi mwaka huu za
kuzikatalia usajili Kampuni za meli za nchi hiyo.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Mkurgenzi Mkuu wa ZMA Abdalla Hussein Kombo
amesema tuhuma hizo zilizotolewa na Mkurugenzi wa Habari na Uchambuzi wa
Taasisi ya NK News kupitia Jarida la NK Pro la Mjini Seoul, Korea
Kusini sio za kweli.
Amesema
ZMA baada ya kupata taarifa ya Azimio hilo iliunda Kamati ya wataalamu
kulifanyia uchambuzi na kutoa mapendekezo kwa Mamlaka juu ya hatua za
kuchukuliwa."Azimio
hilo limetaja majina ya meli 31 za Korea Kaskazini ambazo nchi zote
wanachama wa Umoja wa Mataifa, ikiwemo Tanzania, inazitaka kuzifutia
usajili au kutozisajili," alisema Mkurugenzi Mkuu ZMA.
Aliongeza
kuwa ZMA ilifanya uhakiki wa meli zote zilizosajiliwa na Mamlaka hiyo
na orodha ya meli zilizoainishwa kupitia Azimio hilo na kubaini kuwa
meli moja yenye jina la First Cleam ilikuwa imesajiliwa kabla ya vikwazo
vya usajili wa meli za Korea Kaskazini lakini ikaamua kuifutia usajili.
Amesema
kuanzia wakati huo, Mamlaka haijawahi kusajili meli yeyote ambayo
ilikuwemo katika orodha iliyotolewa na Umoja wa Mataifa na imekuwa
ikichukua tahadhari kubwa katika usajili wa meli.
Mkurugenzi
Mkuu wa ZMA alisisitiza kuwa ili kuhakikisha hawatoi usajili kwa meli
zenye uhusiano na Korea Kaskazini imekuwa ikishirikiana kwa karibu na
Taasisi za Kimataifa ikiwemo IMO.
Hata
hivyo amekiri kuwa Kampuni ya Filtex ambayo ilikuwa wakala wa ZMA
nchini Dubai na kuvunja naye mkataba bado inaendelea kusajili meli kwa
jina la Zanzibar kinyume na sheria.
Amesema
tayari wameshawasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuifuatilia
Kampuni hiyo na kuifungulia mashtaka kwenye mahakama za Kimataifa.Amesema
katika kukabiliana na uharamia unaofanywa na Kampuni ya Filtex, miezi
michache ijayo, ZMA itafungua Ofisi yake nchi Dubai kwa ajili ya usajili
wake wa meli wa Kimataifa.
Kufuatia
majaribio ya Korea Kaskazini kutengeneza silaha, Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa katika kikao chake cha 7638 kilichofanyika tarehe 2
Machi, 2016 ilipitisha Azimio la kuiongezea vikwazo Korea Kaskazini
ikiwemo kuzinyima usajili meli zote za nchi hiyo ama zenye uhusiano
nazo.
No comments:
Post a Comment