Abiria wakiteremka katika Kivuko cha Mv Kome II kinachotoa huduma kati ya Nyakarilo na Kome wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Na Theresia Mwami TEMESA Mwanza
MTENDAJI
Mkuu TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amemuagiza Meneja wa TEMESA Mwanza
Mhandisi Ferdinand Mishamo kuwafuta kazi mara moja watumishi sita wa
kivuko cha Mv Kome kuanzia 11/10/2016 pamoja na kuwapa onyo kali
watumishi wengine wawili wa kivuko hicho kwa kuondoka katika eneo la
kazi bila ruhusa ya mkuu wao wa kazi.
Ametoa
agizo hilo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha
TEMESA mkoani Mwanza na kutembelea kivuko cha Mv Kome kinachotoa huduma
ya usafiri kati ya Kome na Nyakarilo Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Dkt
Mussa Mgwatu pia amemwagiza Meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Ferdinand
Mishamo kuhakikisha wafanyakazi wa karakana na kivuko wanawajibika
ipasavyo ili kuondoka na uzembe kama uliojitokeza.
“Hatuwezi
kuvumilia uzembe namna hii watumishi wanaamua tu kuondoka eneo la kazi
bila kupata ruhusa kutoka kwa wakuu wao hii sio sawa kabisa na nakuagiza
Meneja hawa watumishi waache kazi mara moja” alisisitiza Dkt Mgwatu.
Aidha
Dkt Mussa Mgwatu amemwagiza Meneja wa TEMESA Mwanza kuajiri watumishi
wengine ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kuzingatia weledi na
uwajibikaji wawatumishi watakao waajiri.
Kwa
upande Meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Ferdinand Mishamo alikiri kuwa
hakukuwa na ruhusa yoyote ya maandishi iliyotolewa kwa watumishi kutokuwepo kazini siku hiyo.
“Mtendaji
sina barua yoyote kutoka kwa watumishi hawa iliyofika kwangu kuomba
ruhusa ya kutokuwepo katika kituo cha kazi.” alisisitiza Mhandisi
Mishamo.
Mhandisi Ferdinand Mishamo amewaja watumishi waliachishwa kazi kuwa ni walinzi
wanne Bw. Apolinary Kapulula, Bw. Marwa Nchagwa , Bw. Msomi Stanley na
Joseph Mtokambali, wengine ni Bw. Baharia Geofrey Biseko na Mkusanya
Mapato wa kivuko hicho Bw. Elisha Mbondo.
Amewataja
Watumishi wanaopewa onyo kali ni Mkuu wa Kivuko cha Mv Kome Bw.Elias
Mabushi na dereva wa kivuko hicho Bw.Juma Bugingo.
Dr.
Musa Mgwatu yupo katika ziara ya kutembelea vituo vya TEMESA vilivyopo
Kanda ya Ziwa ili kubaini changamoto zilizomo na kuzitafutia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment