TAASISI
isiyo ya kiserikali ya Mathayo Suleiman Foundation yatoa msaada wa
vyakula katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira
magumu cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza
baada ya kukabidhi msaada huo Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo
Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman, amesema kidogo walicho nacho
kinaweza kuwasogeza siku mbili tatu watoto wanaoishi katika kituo hicho
kwani kinakabiliwa na uhaba wa chakula kwa kiasi kikubwa sana.
Pia
amesema kuwa katika maisha tumetofautiana ndio maana wanachama wa
taasisi hiyo wameona watoe kile kidogo walichokuwa nacho kwani kila mtu
anakula kwa urefu wa kamba yake.
Nae Mratibu wa Kituo cha
Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es
Salaam, Isa Buzohera amewashukuru wanachama wa Taasisi hiyo kwa kutoa
mchango wao kwani taasisi ilikuwa katika hali mbaya sana ya ukosefu wa
chakula.
Amesema kuwa kituo hicho Dogodogo
Maltiporpuse Training Centre mpaka sasa kinawatoto 39 wasichana 10 na
wavulana 29 amesema kituo hicho Kilifunguliwa 2003 kwa lengo la kuwapika
kiufundi watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze
kujitegemea wakiwa na nyenzo mhimu ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Amesema
kuwa uhaba wa chakula ukiendelea kituo hicho kitafungwa kwani mpaka
sasa wanahitaji zaidi ya Milioni 205 kwaajili ya chakula pamoja na vifaa
vya kuwapa kila mhitimu wa mafunzo yanayotolewa katika kituo hicho.
Mwenyekiti
Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman
(Mwenye suti nyeusi katikati) akikabidhi mbuzi kwaajili ya nyama kwa
Mwalimu wa kituo cha Dogodogo
Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam,
Rosemary Nyabuzuki leo. Wengine ni wanachama wa Taasisi ya Mathayo
Suleiman.
Mratibu
wa Taasisi ya Mathayo Suleiman, Banga Suleiman(Mwenye Suluali Nyeupe)
akishirikiana na wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation
wakikabidhi unga kwa watoto wa kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanachama wa taasisi ya Mathayo suleiman wakikabidhi msaada kwa watoto wa kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo.
Mratibu wa Kituo cha
Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es
Salaam, Isa Buzohera akiwashukuru wanachama wa Taasisi ya Mathayo
Suleiman kwa jinsi walivyojitoa katika kuchangia kituo hicho msaada wa
chakula pamoja na vitu mbalimbali.
Wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha Dogodogo
Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo
mara baada ya wanachama hao kutembelea katika kituo hicho na kujionea
baadhi ya Shughuli zinazofaywa na watoto hao katika kituo hicho.
Wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman wakimsikiliza Mratibu wa Kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, Isa Buzohera katika kituo hicho leo.
Mwenyekiti
Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman
akizungumza mara baada ya kupata maelezo ya kituo cha Dogodogo
Multiporpuse Training Centre.
Mwenyekiti
Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman
akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika kituo cha
Wanachama
wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman
wakiangalia meza ya kukunja na kukunjua walipotemelea katika Darasa la
uchongaji Vitu vya Samani walipotembelea katika kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salam leo.
Wanachama
wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman wakipata
maelezo walipotembelea katika darasa la ushonaji nguo kwa watoto wa
kituo cha Dogodogo Bunju jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman
akiwa na wanachama wa taasisi hiyo wakiangalia ngoma inayochezwa na
watoto wa kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre jijini Dar es Salaam leo.
Wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman wakitembelea mabweni ya watoto hao.
Watoto walio katika Kikosi cha Zima moto katika kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre wakifanya mazoezi ya kuzima moto endapo kukitokea tatizo la nymba kuungua.
Kikosi cha Zima moto katika kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre wakiwa katika picha ya pamoja.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Mathayo Suleiman wakiwa katika picha ya pamoja na Watoto walio katika Kikosi cha Zima moto katika kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre jijini Dar es Salaam leo.
Watoto walio katika Kikosi cha Zima moto katika kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre jijini Dar es Salaam leo wakimuokoa mtu aliye juu ya ghorofa wakati wa tatizo la Moto.
Mtu aliyekuwa juu ya Ghorofa mara baada ya kupata msaada wa kutolewa eneo la Tatizo la Moto.
No comments:
Post a Comment