Mwashungi Tahir na Fatma Makame/Maelezo Zanzibar
Waziri
wan chi ofisi ya makamo wa pili ya rais Mohammed Aboud Mohammed amesema
uchumi wa Zanzibar unazidi kuimarika kwa karibu ya asilimia saba na
mfumuko wa bei bado upo kwenye tarakimu moja na pato la Taifa
linazidi kukua.
Ametoa
maelezo hayo ofisini kwake Vuga wakati alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi
Serikali ya awamu ya saba kipindi cha pili cha uongozi wa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein.
Amesema
katika awamu hii kwa ujumla harakati za uchumi zinaendelea vizuri na
ishara zote za kuimarisha uchumi katika mwaka huu wa fedha zinatoa sura
nzuri za mafanikio.
Akizungumzia
suala la Muungano amesema unaendelea kuimarika na vikao mbali mbali
vya watendaji wakuu wa pande mbili wakiwemo mawaziri vimeshafanyika na
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ameshafanya vikao viwili vya
kisekta kwa nia ya kutatua changamoto zilizopo.
Waziri
Aboud ameelezea kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekamilisha
kazi ya kuipandisha hadhi iliyokuwa Idara ya upigaji chapa na mpigaji
chapa mkuu wa serikali na kuwa wakala wa serikali wa uchapaji.
Aidha
amesema kazi ya kufunga mitambo mipya ya uchapaji imekamilika na
mafundi wa kiwanda hicho wanaendelea kupatiwa mafunzo ili kuimudu
teknolojia mpya ya mitambo hiyo ili kuongeza ufanisi na kuongeza
upatikanaji wa huduma bora na kwa wakati.
Sambamba
na hayo Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kupitia Tume ya kitaifa ya
kuratibu na udhibiti madawa ya kulevya imepania kutoa athari za madawa
ya kulevya kwa jamii.
Hivyo
Tume hiyo imefanya kikao maalum na maofisa na wapelelezi wa Jeshi la
Polisi wa Mikoa na Wilaya za Unguja kilichoongozwa na mkuu wa Mkoa
Mjini Maghribi kuweka mikakati dhidi ya uingizaji na usambazaji wa
madawa ya kulevya .
Mh
Aboud amesema ofisi yake inashirikiana na Ofisi ya ukaguzi na mdhibiti
mkuu wa Serikali kuendesha zoezi la uhakiki wa wafanyakazi wa Ofisi ya
Makamo ya Pili ya Rais na Taasisi zake ili kubaini wafanyakazi hewa.
“Katika zoezi hili imebainika kwamba Ofisi yetu hakuna wafanyakazi hewa kama inavyobainika sehemu nyengine" alisema wazirihuyo.
Aidha
amesema Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais bado itaendelea kufanya kazi
kwa bidii , ufanisi na tija ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Amesisitiza
kuwa mambo muhimu ya kuzingatiwa hivi sa kwa nchi yetu ni kuimarisha
uzalendo na kusimamia matumizi bora ya ardhi kwani watukishirikiano
katika masulala hayo tutaweza kudumisha amani na upendo na kupiga hatua
zaidi ya maendeleo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akitoa
tarifa ya mafanikio ya Ofisi yake kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya
chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha pili cha uongozi wa Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein Ofisini
kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Wandishi
wa habari wakifuatilia tarifa ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa na mazungumzo nao Ofisini
kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed
alipokuwa akijibu maswali ya wandishi wa habari katika Mkutano wake
Ofisini kwake Vuga.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment